Na Talib Ussi, Zanzibar
Chama cha ACT Wazalendo
kimezitaka Benki ya Dunia na IMF kusimamia vyema nafuu ya madeni iliyotolewa na nchi
za G20 kwa nchi zinazoendelea
kuhakikisha zinakuwa na mpango madhubuti wa kuigeuza nafuu hiyo kuwa fursa ya
maendeleo ya watu na sio ya vitu.
Kauli hiyo ilitolewa na
Mwenyekiti wa chama hichoMaalim Seif Sharif Hamad Vuga Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa nchi
zenye uchumi mkubwa duniani ( G20) zimekubali kusimamisha malipo ya madeni ya nchi zinazoendelea ili ziweze
kujipanga katika kupambana na Janga la maradhi ya Corona.
Alivitaka vyombo hivyo
viwili kuhakikisha nchi zote ambazo zitapata nafuu hiyo lazima waonyesha mpango unaotekelezeka wa kuimarisha sekta ya
afya kwa upana wake.
“Lazima nchi hizo
zionyesha mfumo wa uwajibikaji ili kuzuiya ubadhirifu na matumizi mabaya ya
fedha” alieleza Mwenyekiti huyo.
Itakumbukwa Maalim Seif
aliziomba nchi za G20 kusimamisha madeni
kwa nchi zinazoendelea ili zijipange vizuri katika kupambana na janga la
maradhi ya korona hapo tarehe 4 april mwaka huu kupitia vyombo mbali mbali.
“Nimeupokea kwa furaha
uwamuzi wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani wa kusimamisha madeni yao kwa
maslahi mapana ya kuwapa nafasi nchi hizo kupambana na janga hili lililotuingia
Duniani kote” alieleza Maalim Seif.
Alisema uwamuzi huo
ulichukuliwa juzi 15 April 2020na kufahamisha kuwa ni uwamuzi wa kihistoria
unaojali maslahi mapana ya kihistoria.
Maalim Seif akitoa
maombi hayo alifahamisha nchi hizo kuwa nchi kama Tanzania inatumia tsh
trilioni 4 kila mwaka kulipia madeni ya
nje na Nchi za G20 jana zimeeleza
zitastisha malipo ya madeni kuazia 1 may 2020 mpaka mwisho wa mwaka huu.
“Ni jambo la kushukuru
sana kwani si haba, kwani itatusaidia sana
kukabiliana na athari za janga la korona” alieleza Maalim Seif.
Sambamba na hilo malim
Seif akijinasibu kuwa chama chake ni chama pekee kilichongoza katika juhudi za kuipata nafuu
pia kitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha
fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliokusudiwa na kwamba zitakaguliwa na
taasisi huru ili kudhibiti mianya ya matumizi mabaya.
No comments:
Post a Comment