HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 03, 2020

TMDA WAKABIDHI MICHORO YA JENGO LA OFISI YAKE KANDA YA KATI DODOMA KWA NHC

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (kulia) akimkabidhi michoro ya ujenzi wa jengo la ofisi za TMDA Jijini Dodoma,  Mhandisi Haikamen Mlekio wa NHC.
Mkandarasi wa NHC, Mhandisi Haikamen Mlekio (kulia) akiwa katika eneo Ilazo katika kiwanja cha patakapojengwa ofisi za TMDA Kanda ya Kati Dodoma.
 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TMDA) inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la ofisi yake kanda ya Kati Dodoma, ujenzi huo unatarajia kuchukua miezi 12, toka18 Aprili 2020 na kutarajia kukamilika 17 Aprili 2021.

Akikabidhi michoro ya ujenzi wa jengo hilo litakalojengwa eneo la Ilazo jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA,  Adam Fimbo kwa Mkandarasi wa Shirika la Nyumba (NHC), Injinia Haikamen Mlekio alieleza kuwa:

Kukamilika kwa ujenzi huu kutaiwezesha TMDA kutekeleza majukumu yake kiufanisi katika kuhudumia mikoa ya Kanda ya kati ambayo inajumuisha Dodoma, singida na Morogoro.

Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na mtaalam Mshauri toka Chuo cha Ardhi, Bi. Neema Mbwambo na wadau wengine wakiwemo wafanyakazi wa TMDA.

TMDA ambayo hapo awali ilijulikana kama TFDA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kusimamia ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

 Lengo la taasisi hii ni kulinda afya ya Jamii dhidi ya madhara yanayoweza kutokea baada ya matumizi ya bidhaa husika.

No comments:

Post a Comment

Pages