Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akizungumza katika kikao cha Wadau wa Afya cha kujadili
utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa wa Songwe
ambapo ameagiza elimu Zaidi itolewe.
Wadau wa Afya
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili
utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa wa Songwe
ambapo imeagizwa elimu Zaidi itolewe.
Katibu Tawala Mkoa wa
Songwe, David Kafulila, akizungumza katika
kikao cha Wadau wa Afya kujadili utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi
vya Corona kwa Mkoa wa Songwe ambapo imeagizwa elimu Zaidi itolewe.
Na Nwandishi Wetu
Mpaka sasa hakuna dawa
wala chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona hivyo njia bora ya kupambana na
ugonjwa huo ni utoaji wa elimu juu ya tahadhari za kujikinga ili mtu asipate
ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe Elimu hiyo bado haitoshelezi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameyasema hayo wakati wa kikao cha Wadau wa Afya
waliokutana mapema leo kujadili utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya
Corona kwa Mkoa wa Songwe.
Brig. Jen. Mwangela
amesema hadi sasa kuna maeneo bado wananchi hawajapata elimu ya tahadhari ya
kujikinga na virusi vya Corona huku akiwaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na
Waganga Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wote.
Amesema elimu itolewe kwa
kutumia vyombo vyote vya habari vilivyopo na kwa namna zote bora ambazo
zitawezesha kuwafikia wananchi wote na kwa wataalamu wa afya ambao baadhi yao
bado hawana elimu hiyo.
Brig. Jen. Mwangela
ameongeza kwa kulitaka Jeshi la Polisi Mkoani Songwe kuendelea kufanya ukaguzi
katika mabasi yote endapo yanazingatia tahadhari za kujikinga na Ugonjwa wa
Virusi vya Corona pia wananchi wote waepuke mikusanyiko isiyo ya lazima.
Amesema taasisi zote
ziendelee kuchukua hatua za tahadhari zilizo elekezwa na wataalamu wa Afya huku
akimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za haraka kutokana na kuwa maji ya
kunawa katika geti la kuingilia Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa yalikua hayana
dawa hali ambayo sio sahihi.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Dkt Hamad Nyembea amesema atahakikisha tahadhari za kujikinga na
Ugonjwa wa Virusi vya Corona zinachukuliwa katika hospitali Teule ya Rufaa ya
Mkoa wa Songwe huku akieleza kuwa tayari wameweka utaratibu wa kupima jotoridi
watu wote wanaoingia hospitalini hapo.
Dkt Nyembea amesema hapo
awali watu wengi walikua wakichukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Virusi vya Corona na Kufuata
maelekezo ya wataalamu wa Afya lakini sasa baadhi wameanza kupuuzia hivyo
anawasihi wasifanye hivyo kwani ugonjwa huo bado ni tishio.
Kwa upande wake Katibu
Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema Mkoa wa Songwe ni lango kuu la
kuingilia na kutoka katika nchi za SADC hivyo hatua za tahadhari juu ya Corona zinazo chukuliwa zinapaswa kuwa
madhubuti Zaidi kuliko maeneo mengine.
No comments:
Post a Comment