Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela, akipokea vitakasa mikono kutoka kwa Balozi wa
Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto ambapo Wizara ya Afya
imetoa vitakasa mikono lita 150 kwa Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akipokea vitakasa mikono kutoka kwa Balozi wa
Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto ambapo Wizara ya Afya
imetoa vitakasa mikono lita 150 kwa Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia
bila kushika koki ambapo Wizara ya Afya imetoa mashine hizo mbili kwa Mkoa wa Songwe, moja itawekwa katika
Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia bila kushika koki ambapo Wizara
ya Afya imetoa mashine hizo mbili kwa Mkoa wa Songwe, moja itawekwa katika
Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Songwe George Kyando akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia bila
kushika koki ambapo Wizara ya Afya imetoa mashine hizo mbili kwa Mkoa wa Songwe,
moja itawekwa katika Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Songwe.
Kutoka Kushoto ni Katibu
Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George
Kyando, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela na na Mkuu wa
Kitengo cha Maji Salama na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike
Mwakitalima wakionyesha mikono baada ya kunawa mapema leo.
Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetoa vifaa mbalimbali vya kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa
wa Songwe huku ikiridhishwa na namna ambavyo Mkoa umechukua tahadhari dhidi ya
ugonjwa huo.
Hayo yamebainishwa mapema
leo na Mkuu wa Kitengo cha Maji Salama na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya
Afya Anyitike Mwakitalima wakati akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe vitakasa
mikono lita 150, mashine za kutolea vitakasa mikono 30 na mashine mbili za
kunawia bila kushika koki.
Mwakitalima amesema Wizara
ya Afya inaendesha Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama ambapo pamoja na
kutoa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona kama vile vitakasa
mikono pia hutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na Corona hasa kwa Mikoa
iliyoko Mipakani kama Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameipongeza Wizara ya Afya kwa kutoa vifaa hivyo
hasa kwa Mkoa wa Songwe ambao upo Mpakani na ni Lango la kuingilia nchi za SADC
ambapo vitakasa mikono 50 vinapelekwa katika jeshi la Polisi na 100 katika halmashauri
zote.
Brig. Jen. Mwangela amesema,“Sisi
Songwe ni Lango la SADC tukizubaa, tusipotoa elimu vizuri kwa Wananchi, tusipo
chukua tahadhari ya kutosha tunaweza kuingiza Ugonjwa kutoka nchi jirani ambazo
nazo zimeahirika na Corona”.
Ameongeza kuwa mpaka kufikia
jana jumla ya wasafiri 180 wamewekwa karantini katika Halmashauri za Tunduma na
Ileje kwa muda wa siku 14 ikiwa ni jitihada
za Serikali katika kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Corona ambapo pia hakuna
mshukiwa wa ugonjwa huo kwa Mkoa wa Songwe hadi sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Songwe George Kyando ameishukuru Wizara ya Afya kwa kutoa kipaumbele kwa Jeshi
hilo kwa kuwapatia vitakasa mikono kwakuwa wamekua wakisahaulika na wadau
wengine huku akieleza kuwa anaendelea kutoa elimu kwa askari wachukue tahadhari
zote muhimu wawapo katika majukumu yao.
Amesema katika mapambano
dhidi ya Ugonjwa wa Corona Jeshi la Polisi lina mchango mkubwa katika kulinda
karantini na maeneo waliyotengwa wagonjwa wa Corona, pia kukagua mabasi na
magari yote ya abiria hivyo wako katika hatari ya kuambukizwa.
Balozi wa Kampeni ya Mikono
Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amesema vita ya
kupambana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona inahitaji ushirikiano wa wananchi
wote waweze kunawa kwa maji tiririka na sabuni kila wakati bila kuchoka na
kutoona kama adhabu.
Mpoto amesema wananchi wa
Songwe wanapaswa kuacha mila za kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana,
kubusiana kuepuka misongamano isiyo ya lazima kwa kuwa mafanikio yatapatikana
kwa umoja ikiwa wananchi wote watazingatia kauli mbiu ya Jilinde na Umlinde Mwenzio.
No comments:
Post a Comment