Mkuu wa Wilaya ya Songwe
Samuel Jeremia Opulukwa akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza
itakayotumika kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani hapo wakati
Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari katika mapambano
dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig.
Jen. Nicodemus Mwangela akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza
itakayotumika kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani hapo wakati
Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari katika mapambano
dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig.
Jen. Nicodemus Mwangela, akizungumza na bodaboda wa kituo cha Stendi ya Mkwajuni
Songwe ambapo amewaelekeza kukaa mbalimbali, kunawa kwa maji na sabuni ili kuchukua
tahadhari dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona.
Na Mwandishi Wetu
Watu wote ambao hawachukui
hatua za tahadhari za kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya
Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa kutofuata maelekezo ya wataalamu wa Afya, watatozwa
faini kwakuwa wana hatarisha maisha yao na ya wengine.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe
Samuel Jeremia Opulukwa amebainisha hayo jana mara baada ya Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Songwe kufanya ukaguzi wa utayari wa kukabiliana na maambukizi
ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona katika Wilaya hiyo.
Opulukwa amesema, “Sasa
tunaanza kutoza faini wote wasiofuata maelekezo ya wataalamu wa Afya kuhusiana
na Corona, mfano tukipita dukani au sehemu ya biashara na hakuna maji na
sabuni, tuta toza faini na kufunga kwa mda biashara hiyo mpaka mtu huyo azingatie
maaelekezo hayo”.
Ameongeza kuwa lengo la
Wilaya hiyo ni kuhakikisha kuwa mahali pa kufanyia biashara ni salama kwa wafanyabiashara
na watumiaji wa huduma hizo huku akieleza kuwa wanawa fuatilia wageni wote
wanao toka nje ya wilaya waliopo katika nyumba za kulala wageni na kuchukua
maelezo yao kwa ajili ya tahadhari endapo wana dalili za Ugonjwa wa Virusi vya
Corona.
Opulukwa ameongeza kuwa
elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wote wa Wilaya ya Songwe hususani katika
maeneo ya migodi ambapo kuna mikusanyiko ya watu wengi pia ameielekeza kamati
inayohusika kutoa elimu ifanye ufuatiliaji wa kina endapo wananchi wanazingatia
wanayo waelekeza.
Aidha amesema mara baada
ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kufanya ukaguzi wa utayari wa Wilaya hiyo
katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona, Kamati hiyo imebaini
baadhi ya mapungufu ambayo kama wilaya itasimamia kuyarekebisha.
Amefafanua kuwa yote
yaliyoonekana kama mapungufu yapo ndani ya uwezo wa Wilaya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
eneo la kuwatenga washukiwa wa Corona lina vitanda vya kutosha na kujenga kichomea
taka katika Zahanati ya Saza ambayo itatumika kutibu wagonjwa wa Corona.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Songwe Dkt Humphrey Masoke amesema wameshaagiza vifaa kinga na tiba vyote
muhimu katika Bohari kuu ya Dawa ili kuongezea katika vifaa vichache walivyo
navyo tayari.
Dkt. Masoke ameongeza kuwa
wana endelea kutoa maelekezo na elimu kwa jamii juu ya tahadhari ya ugonjwa wa Virusi vya Corona
kwakuwa bado baadhi ya wananchi wanaamini ugonjwa wa Corona ni wa wazungu hivyo
hauwahusu.
Estin Nyangito Mkazi wa
Mkwajuni Songwe amesema wamesha pewa elimu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga
na Virusi vya Corona na elimu hiyo wataisambaza kwa wananchi wengine ili nao
waweze kuchukua tahadhari.
Kwa upande wake Jakson
Mwampashi Mkazi wa Songwe amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuweka utaratibu wa
kutoa elimu mara kwa mara na kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia
magari ya matangazo ya barabarani ili wananchi wote waweze kupata elimu ya
Corona
No comments:
Post a Comment