Watumishi wa BVR Oparetas Kts na waandishi wasaidizi wakiwa kwenye mafunzo ya
namna ya kutumia mashine hizo pindi watakapokuwa kwenye majukumu ya kuwahudumia wananchi
watakaofika kuhakiki taarifa zao ili waweze kupata kitambulisho cha mpiga kura.
Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanza
zoezi la uboreshaji awamu ya pili wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye ndio Afisa mwandikishaji, Aron
Kagurumjuli amesema wamejipanga vilivyo katika uboreshaji huo.
Kagurumjuli
ametoa kauli hiyo wakati wamafunzo ya kuwajengea uwezo mbalimbali kuhusu namna
kuwahudumiwa wananchi wanaokuja kuboresha taarifa zao sambamba na namna ya kutumia
mashine wakati wa kuchukua picha kwa ajili ya kutoa vitambulisho.
Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri hiyo
imejipanga vizuri katika mchakato huo na kwamba inategema matokeo mazuri ya
mwitikio wa wananchi kama ilivyokuwa kwa awamu ya kwanza kutokana na kuwepo kwa
ushikiano madhubuti baina ya AROKATA pamoja na watendaji wengine wa Hamashauri hiyo.
Ameongeza
kuwa mchakato huo ni mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi vitambulisho vyao
na kuwataka wale ambao walipitwa na mchakato huo kwa awamu ya kwanza kujitokeza
sasa ili waweze kupata vitambulisho vyao.
“ Nawapongeza wote mliopata nafasi hii, kiapo
mlichokula hapa ni cha uaminifu na uadilifu, mnakwenda kuwahudumia wananchi,
niwasihi hatuhitaji muende kinyume na maelekezo ambayo mnapewa na watalaamu
wetu kwenye mafunzo haya, wahudumieni wananchi vizuri” amesema Kagurumjuli.
Aidha
Kagurumjuli amewataka watumishi hao kuzingatia maelekezo wanayopewa na
watalaamu kuhusu namna ya kumuhudumia mwananchi hasa katika kipindi hiki cha
ugonjwa wa mlipuko wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya COVID 19
(Corona) ikiwemo kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupaka vitakasa
mikono (Sanitizer).
Amesema kuwa
katika kila kituo kutakuwa na watu ambao watakuwa ni mahususi kwa ajili ya
kuwanawisha mikopo pamoja na kuwapaka vitakasa mikono ili kuwakinga na
maambukizi ya ugonjwa huo.
Kagurumjuli
amefafanua kuwa zoezi hilo la uandikishaji litaanza rasmi Mei mbili na
kumalizika Mei Nne mwaka huu na kwamba wote ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha
awamu ya kwanza wanaruhusiwa kwenda kwenye vituo vyao kwa ajili ya
kujiandikisha.
No comments:
Post a Comment