HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 13, 2020

MATATANI KWA KUKUTWA NA SARE ZA JWTZ



Na Lydia Lugakila, Kagera

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na sare za  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alizovaa kutokea mkoani Arusha kwa kile kilichotajwa kuwa ni  ukwepaji nauli katika basi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa kijana huyo alikamatwa akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni, eneo la Kamachumu wilayani Muleba, na kuwa alipohojiwa amekiri kuiba sare za baba mkwe wake, ambaye ni askari wa JWTZ mkoani Iringa na kujifanya ni askari wa Jeshi hilo kikosi cha mizinga mkoani Arusha.
Mtuhumiwa huyo amesema kuwa sababu zilizomfanya anafika mkoani Kagera ni kumfuata mpenzi wake aliyempata hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii na kuwa alipofika mkoani hapa hakubahatika kukutana naye ndipo alipoanza kufanya utapeli ili apate nauli ya kurudi alipotoka

No comments:

Post a Comment

Pages