HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 07, 2020

MTOTO ASOMBWA NA MAJI KAGERA

Na Lydia Lugakila, Kagera

Mtoto  mmoja aliyetambulika kwa jina ya Mariam Burhani mwenye  umri wa miaka 13 mkazi wa kijiji cha Bunazi kata ya kasambya wilayani missenyi mkoani Kagera amepoteza maisha baada ya kuzama katika dimbwi la maji.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Christopher Kamwoma, mtoto huyo amezama maji Mei 5 mwaka huu majira ya saa 9 jioni wakati akijaribu kuvuka maji hayo.

Kamwoma ameongeza kuwa baada ya mtoto huyo kuzama majirani walijitahidi kumtafuta bila mafanikio hadi mwili wake ulipopatikana Mei 6 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bunazi, Mwesigwa Kashangaki, amewataka wazazi kuhakikisha hawawaruhusu watoto wao kucheza karibu na maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kwani maeneo hayo siyo salama kwa kipindi hiki.

No comments:

Post a Comment

Pages