NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Tabora (Uyui) imetoa mikopo ya
shilingi milioni 43 kwa vikundi13 kwa ajili ya kuviwezesha katika uzalishaji
mali.
Mikopo hiyo imekabidhiwa kwa vikundi jana na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Aggrey Mwanri kwa niaba ya Halmashauri hiyo wakati wa kikao cha Baraza Madiwani.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hemed Magaro alisema
kuwa wametoa kiasi cha shilingi milioni 19 kwa vikundi sita vya wanawake,
vikundi 6 vya vijana vimekopeshwa milioni
19 na kikundi kimoja cha walemavu kimekopeshwa shilingi milioni 5.
Alisema mkopo huu unafikisha shilingi milioni 135.5 ambazo
zimeshatolewa katika vikundi kama sehemu asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri alivitaka vikundi
vilivyokopeshwa kuhakikisha wanatumia fedha za mikopo walizopata katika
shughuli za uzalishaji mali kwa ajili ya kuboresha maisha yao.
Alisema fedha walizokopehwa ni lazima wazirejeshe katika muda
waliokubaliana na uongozi wa Halmashauri ili ziweze kusaidia vikundi vingine.
No comments:
Post a Comment