Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi
Stella Manyanya (kulia) akiwa na Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano
Mhandisi, Atashasta J Nditiye {aliyeva koti jeusi} pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) wakiwa katika katika shughuli ya mapokezi ya
ndege ya Ethiopia Airlines iliyoanza
safari zake kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza
kuchukua minofu ya samaki za kilogram 17,262. Tarehe 21 mei 2020 . Picha
na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara.
Ndege ya Ethiopia
Airlines iliyoanza safari zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa
Mwanza kuchukua minofu ya samaki na imepakia
kilogram 17,262 zenye thamani ya Tsh. 191,874,837.78 na mrabaha uliolipwa ni
Tsh. 9,541,301.21. Tarehe 21 mei 2020.
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza wakiandaa
mizigo ambayo ni minofu ya samaki ya kilogram 17,262 iliyosafirishwa na Ndege
ya Ethiopia Airlines iliyoanza safari
zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa Mwanza kuchukua minofu ya samaki. Tarehe 21 mei 2020.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi
Stella M. Manyanya (kulia), akikagua uandaaji wa mizigo ya minofu ya samaki ya kilogram 17,262 zenye thamani ya Tsh.
191,874,837.78 iliyopelekwa ndege ya Ethiopia
Airlines iliyoanza safari zake 21 mei 2020 kuja Tanzania katika mkoa wa
Mwanza kuchukua minofu ya samaki. Tarehe
21 mei 2020.
Na Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya ametangaza fursa za soko la samaki
kanda ya ziwa.
Mhe. Manyanya ameyasema hayo
21 mei 2020 katika shughuli ya mapokezi ya ndege ya Ethiopia Airlines iliyoanza safari zake kuja Tanzania
katika mkoa wa Mwanza kuchukua minofu ya
samaki ambao inauzwa katika nchi mbalimbali.
Mhe. Manyanya amesema kuwa "Mpaka
kufikia mwezi machi 2020 samaki Tani 392,933 wamevunwa nchini na mauzo
yameongezeka kulingana na miaka miwili iliyopita ambapo mauzo yalikuwa Bilioni
379 na kufikia bilioni 691.88 kwa mwaka 2018/2019. Tani 32,388.88 zenye thamani
ya Bilioni 436.97 ziliuzwa nje ya nchi na mapato kwa Serikali yalikuwa bilioni
19.1"
Mhe. Manyanya baada ya
kujionea ndege ya Ethiopia Airline ikipakia samaki ametumia fursa hiyo
kuwatangazia na kuwadhihirishia wawekezaji wote nchini kuwa kuna soko la samaki
la uhakika kwasababu kwa sasa samaki zinafatwa moja kwa moja mkoa wa mwanza na
kupelekwa katika maeneo mbalimbali duniani kote.
“Tanzania tumejariwa, tunao samaki
wazuri na wakutosha na sio ziwa victoria tu tuna majiziwa mengine makubwa na
bahari ya hindi, kwa hiyo naomba niwadhihirishie wawekezaji wote kuwa sasa tuna
soko la uhakika la samaki kwahiyo jitokezeni kuwekeza kwasababu minofu yetu ya
samaki inafatwa moja kwa moja na ndege hadi mkoa wa Mwanza”
Aidha amesisitiza kuwa "Ndege
ya Ethiopia iliyoanza kuja leo 21 mei 2020 imepakia kilogram 17,262 zenye
thamani ya Tsh. 191,874,837.78 na mrabaha uliolipwa ni Tsh. 9,541,301.21 na
samaki hizo zitauzwa katika nchi za Belgum, Holand, Germany, France, Portugal
na Australia na kwa upande wa mabondo (fish maws) soko kubwa ni china"
Nae Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi
na Masiliano Mhandisi, Atashasta J Nditiye amesema kuwa safari za ndege ya
Ethiopia kuja kuchukua samaki hapa mwanza ni fursa kubwa kwa wana Mwanza na
Kanda ya ziwa kwa ujumla maana kabla ya hapo ilikuwa inakuja ndege ya Rwanda
Air ambayo ilikuwa inakuja mara moja kwa wiki kila jumanne Lakini Ethiopia
Airlines imeanza safari leo na bado ratiba yake haijajulikana.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhe. John Mongella amesema kuwa ni viwanda vitatu vilinavyosafirisha
samaki leo ambavyo ni (i) Kiwanda cha Victoria Perch limited ambao
wanasafirisha Tani 5.4 (5,400kg) zenye thamani ya USD 21,600 (ii) Kiwanda cha
Nile Perch Limited amabo wanasafirisha
Tani 8.9 (8990kg) zenye thamani ya USD 35,900 (iii) Kiwanda cha Omega Fish limited
kinachosafirisha Tani 5 (5,000kg) zenye thamani ya USD 22,320.
Aidha, Mongella amesisitiza
kuwa Uzakishaji wa kanda ya ziwa kwa wastani kila wiki katika kipindi cha
mavuno ni wastani wa Tani 1100 na kipindi mavuno haba ni tani 220.
No comments:
Post a Comment