HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

May 22, 2020

Prof. Mkumbo “Tunatengeneza vitakasa mikono kwa sababu tunawathamini wafanyakazi na wananchi ambao ndio wadau wetu wakuu katika huduma”

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akionyeshwa utaratibu unaotumika katika kuchanganya Kemikali zinazotumika kuandaa vitakasa mikono katika maabara ya maji jijini Dodoma. Wizara ya Maji katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID – 19) wataalam wake wameweza kutengeza vitakasa mikono kwa ajili ya wafanyakazi na wateja wanaofika maofisini kupokea huduma mbalimbali.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akiangalia vifaa vinavyotumika kupima Kemikali zinazotumika kuandaa vitakasa mikono. Kazi hiyo inayofanyika katika maabara ya maji jijini Dodoma. Mtaalam anayeonyesha ni Mkemia Bw. Samuel Mhadisa wa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akisoma vyeti vya ubora wa bidhaa vilivyotolewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) iliyofanya kazi ya ya kukagua eneo la uzalishaji wa vitakasa mikono na sampuli zilizozalishwa kabla ya matumizi.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akitoa maelekezo kwa timu aliyoiunda maalum ambayo, pamoja na mengine inahakikisha kazi zinafanyika kwa ubora na kiwango kwa wateja wote, na taratibu za wataalam wa afya zinazingatiwa mahala pakazi. Timu hiyo ndiyo iliyobuni wazo la kuzalisha vitakasa mikono kwa kutumia wataalam wa wizara kufuatia mlipuko wa janga la COVID-19.

No comments:

Post a Comment

Pages