HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 21, 2020

Tazama yaunga juhudi mapambano ya Corona

  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, wakati wa hafla ya kupokea sehemu ya msaada wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kutoka Kampuni ya kusafirisha mafuta Tanzania Zambia  ‘TAZAMA Pipelines Limited ’, Abraham Saunyama kwa ajili ya wilaya hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).
  Mkuu wa Idara ya Rasirimali Watu wa Kampuni ya kusafirisha mafuta Tanzania Zambia  ‘TAZAMA Pipelines Limited ’,Deogratius Msemwa, akizungumza katika hafla hiyo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri (kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kutoka kwa Meneja wa Kanda Kampuni ya kusafirisha mafuta Tanzania Zambia  ‘TAZAMA Pipelines Limited ’, Abraham Saunyama kwa ajili ya wilaya hiyo.  

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri (kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kutoka kwa Meneja wa Kanda Kampuni ya kusafirisha mafuta Tanzania Zambia  ‘TAZAMA Pipelines Limited ’, Abraham Saunyama kwa ajili ya wilaya hiyo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya kusafirisha mafuta Tanzania Zambia  ‘TAZAMA Pipelines Limited ".




NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na kupambana na Virusi vya Corona vyenye thamani ya Sh. Milion 35 kutoka Kampuni ya kusafirisha mafuta ya  ‘TAZAMA Pipelines Limited ’ kutoka Tanzania hadi Zambia, zoezi hilo lilifanyika jana katika Ofisi za Mkuu huyo wa Wilaya.

Akipokea vifaa hivyo alisema Kigamboni iko salama na kama Wilaya wamaejipanaga vema kukabiliana na Janga la Corona kuanzia ngazi ya kata hadi Wilaya, ambapo kuna kamati mbalimbali ambazo zinaendesha kampeni ya kutoa elimu na ushauri kwa Wananchi ili kuweza kujikinga na maambukizi ya Corona.

“Kwanza nipende kuwashukuru kampuni ya Tazama kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano ya ugonjwa wa Covid19, juhudi hizi zinaonyesha jinsi gani Serikali yetu chini ya Dat John Pombe Magufuli inavyofanya kazi kwa weledi katika kuhakikisha tunalinda maisha ya Watanzania wote.

“Serikali yetu imejithatiti kuhakikisha kuwa wananchi wote wako salama na sisi kama Wilaya ya Kigamboni tunatekeleza maagizo yote ya Rais, Waziri na wataalamu wa Afya ili kuendana na kasi ya mapambano ya ugonjwa wa Covid19.

“Kwa kuyafanya yote hayo tumeunda kamati mbalimbali ngazi ya kata zetu sawa na kamati za kitaifa kubabiliana na jangat hili, na niwaondoe Shaka kwamba Kigamboni iko salama na tuko imata kukabiliana na janaga hili, niwaombe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote.

“Lakini pia kigamboni sasa shughuli zote zimesharejea, wafanya biashara wote sasa wako huru kuendesha biashara zao, pamoja na hayo Kigamboni ni Wilaya ya Utalii sasa tuko tayari kupokea watalii zaidi ya 1000 kwani tunauwezo wa kuwalinda na kubabiliana na maambukizi yoyote ambayo yatajitokeza.

“Mwisho nipende kuwahakikishia kuwa vifaa hivi vitaenda kutumika kama mabavyo imepangwa, baada ya kuthibitishwa Wataalamu wa Wizara ya Afya kama ambavyo Raisa John Pombe Magufuli ameagiza, kisha vitaweza  kusambazwa katika maeneo yote ambayo mmepanga kuvitoa.”alisema Msafiri.

Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Kanda  wa Kampuni TAZAMA Pipelines Abraham Saunyama alisema TAZAMA Pipelines Limited inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kulikabili janga hili la corona.  Hivyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambao ya corona, TAZAMA Pipelines Limited imetoa vifaa mbalimbali kwa hospitali na kliniki upande wa Zambia.

“TAZAMA Pipelines Limited upande wa Tanzania, leo (jana) tunaanza kutoa vifaa mbalimbali katika mapambano dhidi ya vita ya corona.  Vifaa hivyo ni ndoo maalumu za kunawia mikono, vipima joto (Infrared Thermometer), sabuni ya maji, barakoa na gloves.


“Tunaanza zoezi la kutoa vifaa hivyo, hapa wilaya ya Kigamboni vyenye thamani ya shilingi 4,938,000/- (milioni nne laki tisa thelathini na nane).  Vifaa tiba vya kujikinga na corona vitatolewa pia hospitali ya Tumbi (Kibaha), Kituo cha Afya Chalinze (Chalinze), Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilosa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa, Kituo cha Afya Makambako, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbeya, hospital ya Wilaya Mbozi na Kituo cha Afya Tunduma.  Thamani ya vifaa vyote ni shilingi million thelathini na tano, laki tisa na thelathini elfu (35,930,000/-).”alisema na kubainisha kuwa.

Tunapongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano ya janga la corona, na kwa namna ya pekee tunampongeza Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kuongoza vita hii.  Kutokana na mikakati thabiti,
 tunaishinda vita hii.  Kama alivyohutubia Taifa hapo Jumapili, kuna ongezeko kubwa la kupungua visa vya corona katika mikoa mbali mbali nchini.  Mchango huu kwa taasisi mbalimbali za Serikali ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya corona.”alisema.

TAZAMA Pipelines ni kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Zambia.  Kirefu cha neno TAZAMA ni Tanzania Zambia Mafuta.  TAZAMA ilianza kufanya kazi mwezi Septemba mwaka 1968, ikiwa na jukumu la kusafirisha mafuta ghafi kwenda Zambia kwa njia ya bomba.

No comments:

Post a Comment

Pages