Askofu Almachius Rweyongeza mwenye kanzu
nyeupe pamoja na viongozi wengine wa dini wakiongea na viongozi wenzao
wa dini.
nyeupe pamoja na viongozi wengine wa dini wakiongea na viongozi wenzao
wa dini.
Na Allawi Kaboyo
Viongozi wa mathehebu mbalimbali ya dini wilayani
Karagwe mkoani Kagera wamefanya maandamano ya Amani yenye lengo la kumshukuru
Mhe. Rais Magufuli kwa kuruhusu kuendelea kufanyika kwa ibaada makanisani na
misikitini kote nchini katika kipindi hiki cha mlipuko wa gonjwa hatali la
COVID-19 linalosababishwa na virusi vya Corona.
Maandamano hayo yamefanyika leo yakitokea ofisi za
mkuu wa wilaya hiyo na kupokelewa na mlezi wa kamati ya Amani ya wilaya hiyo
Mwashamu Baba Askofu Almachius Vicent Rweyongeza wa jimbo la katoriki Kayanga
pamoja na mkuu wa wilaya Mhe.Godfrey Muheruka katika viwanja vya nyumba ya
vijana (ANGAZA) wilayani humo.
Kiongozi wa maandamano hayo mwenyekiti wa kamati ya maadili
ya wilaya Karagwe Mchungaji Selesitin John wa kanisa la FPCT Kayanga amesema
kuwa wameguswa na kauli ya Rais magufuli aliyoitoa mei 17 mwaka huu baada ya kushiri ibaada ya
jumapili wilayani Chato.
Amesema kuwa suala la Rais Magufuli kuruhusu
watanzania kuendelea kuabudu kwa kuliombea taifa na janga la Corona kwa
kutofunga nyumba za ibaada linawapa msukumo mkubwa wa kuendelea kumshukuru na
kumombea kwa mungu.
“Sisi
viongozi wa dini wilayani Karagwe tunaungana na Rais Magufuli katika kipindi
hiki cha Corona kuendelea kufanya ibaada huku tukichukua tahathali zote
zinazotolewa na wataalamu wa afya, Magufuli alichaguliwa na mungu kuja kutuokoa
sisi watanzania hivyo tunayo kila sababu ya kumuunga mkono na kuzidi kuliombe
taifa letu libaki salama, niwaombe watanzania tuendelee kumuamini na kumuombea
Rais wetu hili nalo litapita.” Amesema Mchungaji
Selesitin.
Kwaupande wake Askofu Almachius baada ya kupokea
maandamano hayo amewashukuru viongozi hao kwa mshikamano na umoja walioudumisha
kwa maslahi ya wanakaragwe na watanzania kwa ujumla ambapo amesema kuwa kitendo
cha kujitokeza hadharani na kumpongeza Rais Magufuli ni kitendo cha kizalendo nay
eye kama mlezi wao amelipokea kwa nia njema.
Asikofu ameongeza kuwa nchi ya Tanzania ilimuhitaji
mtu kama Rais magufuli ambaye mpaka sasa amekuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa ya
Africa na ulimwenguni kwa ujumla, na kuongeza kuwa kupitia maumbi na dua
zinazoendelea kufanyika katika makanisa na misikiti katika kipindi hiki cha
ugonjwa wa Covid-19 yamelifanya Taifa kuanza kuuepuka ugonjwa huu kama Rais
alivyosema tunaendelea vizuri.
“Tumekuwa
tukimsikia Rais Magufuli akituomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa
na kuwasihi waumini wetu kufunga na kusali tukimuomba mungu wetu aweze
kutunusuru na janga hili, sasa kupitia maombi na dua zetu mungu ameanza
kutujibu ni wajibu wetu kama viongozi wa dini kudumisha Amani na mshikamano
wetu bila kujali mathehebu yetu.” Asikofu Almachius
amesema.
Asikofu amesisitiza kuwa wataendelea kuungana na
Rais kwa kuwasihi waumini wao kufunga na kusali ili kumshukuru mungu kama Rais
alivyotangaza siku tatu za maombezi ya shukurani yatakayofanyika kuanzia ijumaa
ya tarehe 21 hadi jumapili ya tarehe 23 kwa makanisa yote wilayani humo.
Kwaupande wake Alhaji Sheikh Mustapha Muyonga Amiri
wa wilaya Karagwe kutoka taasisi ya kiislamu JASUTA amesema kuwa licha ya
kuwepo kwa janga la Corona waumini wa dini hiyo wameendelea kufanya ibaada
mbalimbali ikiwemo kushiriki vipindi vya swala katika misikiti yao huku
wakichukua tahadhali mbalimbali.
Amesema suala la Rais Magufuli kutofunga nyumba za
ibaada limeliongezea daraja kubwa kwa mungu Taifa hili la Tanzania kwa
uchamungu unaoendelea katika maeneo mbali mbali na kuongeza kuwa janga la
Corona sio janga la kwanza Duniani maana yalikuwepo majanga mengi na makubwa
kabla yetu.
“Kitendo
cha Rais magufuli kuwaacha watanzania waendelee kuabudu ni kitendo cha kishujaa
sana hivyo watanzania kwa imaani zetu tuendelee kumuombea Rais wetu na taifa
letu, Kabla yetu yalikuwepo majanga tena makubwa lakini nyumba za ibaada
hazikuwahi kufungwa hata nyakati za mitume, na mungu alishatwambia katika
kitabu chake kitukufu Qur-an kuwa
niombeni name nitawaitikieni hivyo tuzidi kumuomba na kumshukuru kila siku,
sisi tumefunga na sasa tunaelekea kumaliza mfungo wetu wa mwezi mtukufu wa
Ramadhan na Inshaallah tutaswali na idd tukiwa salama.
Amesema Alhaji Muyonga.
Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka Baada ya
kuwapokea viongozi wa dini amesema viongozi wa dini wilayani humo wamekuwa
mfano wa kuigwa kwa kuhubiri Amani na mshikamano kwa wanakaragwe ambapo
amewahakikishia Amani na usalama wakati wakiliombea taifa.
Muheruka amesema kuwa kuwa mbele kwa viongozi wa
dini katika kuliombea taifa ni jambo la kizalendo kwa nchi yao na hilo ndilo
analolihubiri Rais Magufuli kwa watanzania wote kuendelea kuomba na kusali ili
tuweze kuepushwa na janga la Corona.
“Kwaniaba
ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli mimi Godfrey Muheruka mkuu wa Wilaya ya Karagwe
na wapokea viongozi wa dini waliojitokeza kufanya maandamano ya kumpongeza Rais
Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanya ibaada katika nyumba za ibaada,
niwahakikishi viongozi wangu wa dini sitawaangusha tutaendelea kuwa pamoja
katika mapambano dhidi ya Corona.”
Mkuu huyo ameongeza kuwa wananchi kupitia viongozi
wa dini wandelee kufanya ibaada huku wakifuata taratibu zote zinazotolewa na
wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali na kuongeza kuwa Corona ipo lakini
wanatakiwa kutokuwa na hufu huku akisistiza kuendelea kufanya kazi kwa
kulijenga taifa lao.
“Mimi
niseme tu wapo baadhi ya viongozi walitangaza kufunga makanisa hapa wilayani
suala lililowapelekea wananchi kutishia kulichoma kanisa hilo, lakini
tulivyoona hali hiyo tulijitahidi kuizui hali hiyo na kanisa halikuchomwa,
hivyo nitoe wito kwa viongozi wa dini waacheni waumini wenu wafanye ibaada
maana gonjwa hili ni gonjwa kama magonjwa mengine na sio kila anayeumwa anaumwa
Corona, niwahakikishieni kwa wilaya Kargwe mpaka sasa tupo salama hatuna
mshukiwa wala mgonjwa wa Corona tuendeleeni kuomba na kufanya kazi.”
Amesema Muheruka.
Viongozi hao wamesema
kuwa wataungana na watanzania wote pamoja na Rais Magufuli katika kufanya
ibaada ya Shukrani kwa mungu kwa ambayo itadumu kwa siku tatu kama Rais
Magufuli alivyotangaza kwa lengo la kumshukuru mungu kwa namna anavyolibariki
taifa la Tanzania
No comments:
Post a Comment