Mkuu
wa wilaya ya Kibaha, Assumphta Mshama (kushoto), akizungumza jambo na
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus baada ya
kumalizika kwa utekelezaji wa Kampeni ya Elimisha Kibaha na Benki ya
NMB kukabidhi msaada wa mabati 160 katika hafla iliyofanyika shule ya
sekondari ya Zogowale mkoani Pwani.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi, Josephat Kandege (katikati), akinong'ona jambo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (kushoto), baada ya benki
hiyo kutoa msaada wa jumla ya mabati 160 kwa shule za sekondari Magindu
iliyopata mabati 106 na shule ya sekondari Msagani mabati 54 yote
yakiwa na thamani ya sh5milioni katika hafla iliyofanyika shule ya
sekondari ya Zogowale halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoani Pwani,
kulia ni mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumphta Mshama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege (kulia), na Mkuu wa Wilaya
ya Kibaha, Assumphta Mshama (kushoto), wakisikiliza jambo kutoka kwa
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani CCM, Hawa Mchafu katika hafla ya
benki ya NMB kukabidhi msaada wa mabati na utekelezaji wa kampeni ya
Elimisha Kibaha katika shule ya sekondari ya Zogowale.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege (Mwenye miwani), Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumphta Mshama (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa benki hiyo idara
ya elimu mkoa wa Pwani baada ya benki ya NMB kutoa msaada wa jumla ya
mabati 160 kwa ajili ya shule za sekondari Magindu iliyopata mabati 106
na shule ya sekondari Msagani mabati 54 yote yakiwa na thamani ya
sh5milioni wakati wa hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Elimisha Kibaha
kukabidhi vyumba vya madarasa 32 iliyofanyika shule ya sekondari ya
Zogowale mkoani Pwani,
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege (katikati), akimkabidhi
moja ya vikombe 12 Meneja wa benki ya NMB kanda ya mashariki, Baraka
Ladislaus kulia baada ya kununua katika harambee ya kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa vyenye thamani ya sh240,000 wakati wa hafla ya
utekelezaji wa kampeni ya Elimisha Kibaha kukabidhi vyumba vya madarasa
32 iliyofanyika shule ya sekondari ya Zogowale halmashauri ya wilaya ya
Kibaha mkoani Pwani, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumphta
Mshama.
No comments:
Post a Comment