Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia Morogoro.
Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia mkoani Morogoro.
Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia mkoani Morogoro.
Ofisa michezo Mkoa wa Morogoro, Grace, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
Goba
Roads Runners (GRR) ni Klabu wa wakimbiaji yenye maskani yake katika
viunga vya Goba Jijini Dar es salaam. Wanachama wa klabu ni wakazi wa
sehemu mbali mbali katika wilaya zote za Jiji la Dar Es Salaam na wa nje
ya Dar Es Salaam.
Katika klabu yetu tuna mafunzo mbalimbali katika ngazi tofauti za wakimbiaji.
Tuna
wale wanaoanza yaani (Beginners), kuna wenye uwezo wa kati yaani
(Intermediate), Wenye uwezo wa mbio ndefu au long run na ultra long run
(advanced).
Tukio
hili ilikuwa ni sehemu ya mafunzo kwa mbio ndefu yaani Ultra Run, na
kwa kuwa Klabu ina malengo ya kuendesha Ultra Marathon Juni, 2021, mbio
hii imetumika kama maandalizi.
Mafunzo
haya yamehusisha wakimbiaji toka GRR na klabu nyingine kama vile Moro
Runners Club, Kigamboni Amsha Amsha Club na Wasafi Jogging Club.
Tulipata hamasa kubwa kutoka kwa Moro Runners waliotupokea kutoka Mikese mpaka Morogoro Mjini.
Mbio hii imeleta hamasa kubwa miongoni mwetu na kudumisha mahusiano mazuri baina yetu.
Tunawashukuru
sana wanachama wa klabu waliochangia kufanikisha mbio hii, wanachama
walioshiriki katika kutoa huduma mwanzo hadi mwisho wa mbio, wadhamini
mbali mbali waliotoa michango yao, Jeshi la Polisi Tanzania, Viongozi
wote wa michezo Wilaya ya Ubungo inapotokea klabu, Viongozi wa Michezo
mkoa wa Morogoro na wilaya zake, Chama cha Riadha Taifa na Baraza la
Michezo Taifa waliohakikisha zoezi hili linaenda
ilivyotarajiwa.Waliofika Morogoro walikuwa ni Edson Mwakalukwa, Eng.
Patrick Katemba, Joseph Katembo na Bakari Semeng'anda..Hawa walitumia
Masaa 19:35:25
Wanawake
walikimbia umbali tofauti ambapo aliyekwenda umbali mrefu zaidi
alienda hadi Mdaula, umbali wa km 120, kwa masaa 16:25:31. Jina Arafa
Msalo.
Wengine ni Mariam Mwalim aliyekimbia km 108 na Janeth Mtenga alieenda km 105.
pia kulikuwa na mlemavu wa viungo aitwaje Shukuru Halfan ambaye alikimbia Kilometa 155 kwa muda wa saa 17:20:00.
Wengine walioshiriki kati ya umbali wa kilometa 100 hadi 150 ni
Karim Chang'a, Alfred Malanji, Baraka Konkara, Johnson Mbunda, William Mutahangarwa,
Proches Julius, Benson Luaga, Joshua Kayombo, Modibo Coulibaly, Lister Pakua, Dawson David, Abbas Adam,
GRR Kama GRR hatujawahi kufeliii.
ReplyDelete