Na Janeth Jovin
KAMISHNA Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Suleiman Kova amesema licha ya kuwa amestaafu lakini bado anawapenda watanzania na anahitaji kuendelea kuwatumikia.
Kova amesema katika kuhakikisha hilo linatimia, ameanzisha Taasisi yake Msaada, Majanga na Uokoaji (Sukos Kova) kwa lengo la kuwatumikia na kuwahudumia watanzania pindi wanapopata shida na majanga mbalimbali.
Aidha amewataka wanawake kuacha kukaa nyumbani na kusubilia kuletewa fedha na wanaume zao badala yake wajiingize katika ujasiriamali ili kupate fedha za kuhudumia familia zao.
Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Mtandao wa nguvu ya pamoja ya wanawake ( women Tapo), Kova amesema licha ya kuwa amestaafu lakini bado anaendelea kufanya kazi na watanzania katika nyanja mbalimbali.
"Ni kweli mimi nimestaafu ila bado nawapenda watanzania wenzangu na nataka niwatumikie na ndo maana nimeanzishaa taasisi yangu ya SUKOS ambayo inanifanya niwe karibu na watanzania wenzangu ," amesema
Hata hivyo amesema suala la mwanamke kuwa wajasiriamali si la hiari bali ni la lazima kwa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
"Tena mwanamke usiwe mjasiliamali wa kawaida bali ingia kwenye biashara na upambane kwelikweli ili mnufaike katika maisha yenu pamoja na familia," amesema na kuongeza
"Wakati wa kuwategemea wanaume zenu pekee katika familia zenu za watu watano hadi 10 sasa umepitwa na wakati, ni muhimu kina mama wakaelewa wajibu wao katika kuchangia kipato cha maisha kama wanavyofanya wanawake waliopo kijijini," amesema
Amesema pamoja na ujasiriamali huo, wanawake hao wanapaswa kuwa makini na fedha chache wanazozipata pamoja na masuala yanayohusiana na afya zao hasa kutokana na magonjwa ya milipuko kama corona na kipundupindu.
"Naupongeza uongozi wa TAPO kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kutoa miongozo mbalimbali na uelewa kwa wajasiriamali wanawake ambao sasa wengi wamejitambua na wameanza kupata mafanikio katika maisha yao,
Mwenyekiti wa Women Tapo,Stella Mbaga amesema kutokana na wanawake kuwa na mchango mkubwa katika jamii wameamkuwa kuwaletea vifaa vya kunawa mikono katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
"Msaada huu tumepata kutoka katika Mfuko wa wanawake hivyo tukasema tuwaletee ili nanyi muendelee kujikinga na corona hapa sokoni," amesema

No comments:
Post a Comment