Na Mwandishi Wetu
Rais John Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Ijumaa Julai 24, 2020, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Serikali ya awamu wa tatu Benjamini Mkapa.
Rais Magufuli ametangaza siku hizo za maombolezo leo ambapo amesema katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Rais Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hospitalini jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu mara baada ya kuugua.
No comments:
Post a Comment