Ofisa Uchechemuzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Florence Majani, akizungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari za jinsia.
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya siku moja yalitolewa na TAMWA jana jijini Dodoma.
Na Suleiman Msuya
CHAMA
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimewashauriwa
waandishi wa kuandika habari za jinsia ili kuhakikisha lengo kuwepo
usawa wa kijinsia linatimia nchini.
Ushauri
huo umetolewa na Ofisa Uchechemuzi wa TAMWA, Florence Majani wakati wa
mafunzo kwa waandishi wa habari zaidi ya 20 kutoka katika mikoa ya
Arusha na Dodoma ambao wapo katika Mradi wa Wanawake Sasa unaofadhiliwa
na Mfuko wa African Women Development (AWDF).
Majani
alisema pia mradi huo unahusisha waandishi wa mikoa ya Dar es Salaam na
Zanzibar ambapo wanaamini kundi hilo ni muhimu katika kufikia jamii
hasa wanawake kuhusu ushiriki wao katika shughuli za kijamii, kisiasa na
kiuchumi bila kuwa na hofu ya jinsia yake.
Alisema
kupitia mafunzo hayo waandishi wataweza kuhabarisha taarifa za ushiriki
wa wanawake katika chaguzi, changamoto wanazokabiliana nazo katika
shughuli za kisiasa.
"Mafunzo
haya yanalenga masuala yote ya uchaguzi kama sheria, changamoto na
mengine hivyo wanahabari wakijengewa uwezo watakuwa na upeo mkubwa wa
kuandika habari hizo kwa kina na ufanisi," alisema.
Alisema vyama vya siasa ni chanzo kushindwa kupitisha wanawake kugombea nafasi za uongozi kutokana na changamoto ya rushwa ya ngono na udhalilishaji.
Majani
alisema baadhi ya wanawake wamekuwa hawana nafasi kwenye siasa na
katika ngazi za maamuzi hivyo ni vema juhudi za waandishi kuripoti hayo
zikaongezeka.
Ofisa Uchechemuzi huyo alisema yapo mambo mengi yanayojitokeza katika kushindwa kwa wanawake kwenye uchaguzi zikiwemo gharama za uchaguzi, mfumo dume unaosisitiza uongozi wa kaya tangia awali, udhalilishaji katika uchaguzi na mfumo mzima wa uchaguzi.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku moja Muwezeshaji, Wakili Mary Mwita alitaja ana za udhalilishaji wa kijinsia kuwa ni pamoja na shambulio la mwili, rushwa ya ngono, udhalilishaji wa kisaikolojia na uchumi duni.
Mwita alisema usawa katika uchaguzi umeainisha mapengo ya jinsia katika sheria tano kwa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia kwamba ni pamoja na kutokubaguliwa kwa njia yeyote ile kwenye mchakato wa uchaguzi, haki ya kupiga kura, kuteuliwa, haki ya kufikia na kutumia rasilimali za uchaguzi, kuhabarishwa na kusikilizwa na haki ya kuchaguliwa.
Aliwataka waandishi wa habari kutoa taarifa kuhusu manyanyaso juu ya wanawake sambamba na kujielimisha kuhusu masuala ya jinsia na kuzifahamu sheria zinasemaje kuhusiana na maswala ya jinsia, pamoja na kuchambua masuala ya jinsia katika jamii.

"Katiba
ya Tanzania kuanzia Ibara ya 12 hadi 29 inazungumzia haki za binadamu
kama haki ya kuishi, usawa kwa watu wote, haki ya kumiliki mali, kila
mtu ana haki sawa mbele ya sheria na hatakiwi kubaguliwa na haki
nyingine muhimu.
Tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainishwa msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2) kinakariri kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsi lugha na itikadi za kisiasa," aliswma
Aidha, alisema mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake 1979 unasisitiza kwamba ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.
Wakili Mwita alisema, ngazi ya kanda maridhiano ya mkataba mwaka 2000 iliingizwa na kubainishwa misingi ya usawa wa jinsia katika kifungu cha 4(1) katika makubaliano yaliyofanyika mwaka 2000
Alisema tamko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC2005) liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake katika kuwa asilimia 30 na baadae kupandisha hadi kufikia 5O hali ambayo Tanzania haijafikia kwa sasa.

No comments:
Post a Comment