Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega.
NA JANETH JOVIN
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema kuwa kwa sasa ina wataalamu wa kutosha na mitambo mbalimbali ambayo inawasaidia kutatua kwa haraka na wakati changamoto nyingi zinazohusiana na mambo ya maabara.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Sabanitho Mtega
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja wa maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mtega amesema Serikali imewapatia wataalamu wa kutosha ambayo kila kukicha wamekuwa wakipata ujuzi unaowawezesha kufanya kazi kwa weledi na kujitegemea.
Aidha amesema majukumu ya mamlaka hiyo yametengwa katika maeneo matatu, ambapo eneo la kwanza ni huduma za kiuchunguzi wa sampuli mbalimbali, huduma za kisheria na utoaji wa ushahidi mahakamani.
Amesema katika eneo la huduma za kiuchunguzi wamekuwa wakifanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali kama vile dawa asili, vyakula, kemikali, viwatilifu pamoja na sampuli za mazingira na kuongeza kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo utoa majibu kwa ajili ya kusaidia mamlaka za udhibiti kufanya maamuzi stahiki.
Amesema pia wamekuwa wakifanya uchunguzi wa sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, ambapo baada ya kuchunguza uwasilisha matokeo kwenye mamlaka husika kwa ajili ya maamuzi ya kisheria.
"Pia sisi ni mamlaka ya udhibiti unaosimamia kemikali za majumbani na viwandani hivyo katika hali hiyo kemikali zote zinazoingia nchini lazima sisi kama mamlaka tuwasajili wale wote wanaoziingiza na kutoa kibali kwa ajili ya kusafirisha ndani na nje ya nchi kemikali hizo," amesema
Amesema kwa hali hiyo wamekuwa wakifanya ukaguzi kwa saa 24 kila siku na kuomgeza kuwa wana wakaguzi wao katika kila mipaka nchini kwa ajili ya kuharakisha utoaji wa mizigo na kuangalia kemikali zote zinazoingia nchini zina ubora unaokubalika na zinatumika kwa malengo yaliyoletewa na si vinginevyo.
"Ila bado tunayo changamoto kwenye uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli mbalimbali ambapo wengi wa wadau uleta sampuli kidogo lakini inahusisha vigezo vingi au kuletewa sampuli ambayo ilihifadhiwa bila kufuata utaratibu hivyo tunashundwa kulifanyia uchunguzi kutokana na kutokidhi viwango vya kufanyiwa
"Katika eneo hili tumekuwa tukiwasiliana na wadau na kuwaelimisha kwamba wanapaswa kuleta sampuli nyingine ili tuweze kufanya uchunguzi na kuwapatia majibu," amesema

No comments:
Post a Comment