Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Manfredo Fanti akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Mohamed wakati alipofika katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba.
NA JANETH JOVIN
CHAMA cha Wadau wa Viungo Tanzania (TASPA) kimesema kuwa upatikanaji wa soko viungo katika nchi za jumuiya ya umoja wa Ulaya umechangia kukuza uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 300 hadi 18,000 katika kipindi cha miaka miwili hadi sasa.
TASPA imesema uzalishaji huo umekuwa kutokana na wakulima kuwa na soko la uhakika kwa bidhaa wanazozalisha na kufundishwa namna ya kulima na kufungasha vizuri na kufungasha bidhaa zao.
Hayo yote yamebainishwa jana na Meneja Uendeshaji wa chama hicho, George Kivelege wakati alipotembekewa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Manfredo Fanti katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa yabayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kivelege amesema kukua kwa uzalishaji huo kunatokana na uwepo wa mradi wa miaka minne wa upanuzi wa masoko katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya udhamini wa EU (Markup).
"Mradi huu ulioanza mwaka 2018, umejikita katika mazao manne ambayo ni chai, kahawa, parachichi na viungo, moja ya jitihada ya mradi huu ni kuunganisha na kuvutia wawekezaji kutoka EU pamoja na kuchochea uuzaji wa bidhaa husika katika masoko ya nje.
" Katika eneo la kuchochea uuzaji bidhaa nje, wauzaji na wazalishaji wa Parachichi waliwezeshwa kushiriki katika maonesho ya bidhaa yaliyofanyika Mwezi Februari mwaka huu mjini Berlin, Ujerumani, kufuatia ushiriki wa maonesho hayo washiriki kutoka Tanzania waliweza kutengeneza biashara kwa kiasi kinachokadiliwa kufikia Dola za Marekani Milioni mbili," amesema
Aidha amesema mwezi Desemba mwaka jana, wafanyabiashara wa Viungo kutoka Tanzania waliwezeshwa kushiriki katika maonesho ya biashara yaliyofanyika mjini Paris nchini Ufaransa.
Amesema katika maonesho hayo jumla ya kampuni tano za Viungo kutoka Tanzania zilishiriki, ambapo zilifanikiwa kukutana na wafanyabiashara wapya na kuingia nao makubaliano ya mauzo.
“Viungo ni dhahabu iliyojificha kwa sababu ni zao lililo na faida kuliko lolote kwa bidhaa zake zinavyouzwa kwa mfano vanila kilo moja huuzwa hadi dola 600 na hiriki Kg1 huuzwa hadi Sh105000,” amesema
Kwa upande wa zao linalolimwa sana amesema hutokana na uhitaji wa soko huku akibainisha kuwa kutokana na ubora wa mdalasini unaozalishwa nchini ulifanya mradi wa Markup kulazimika kuwafundisha wakulima namna ya kulilima.
“Tulianza na mdalasini na lengo ilikuwa ni kufundisha wakulima 800 lakini tulifundisha 1300 katika kipindi cha miezi 6 na tulikuwa tumepanga kuanza kufundisha kilimo cha Iriki kutokana na mahitaji tulitaka kufundisha wakulima 2500 lakini kutokana na corona tulishindwa ila tutaanza Septemba mwaka huu katika Mikoa ya Tanga, Morogoro na Mbeya,”
Amesema pia wapo katika mkakati wa kuweka nembo maalumu ambapo bidhaa ikipitishwa na TBS itakuwa ikipigwa nembo maalumu ambayo itamruhusu kuuza bidhaa moja kaa moja nje.
Amesema mpaka sasa wako na jumla ya wanachama 2500 kutoka 154 pamoja na kampuni 58.

No comments:
Post a Comment