WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa
ujumla watumie nyumba za ibada kuhubiri suala la amani na utulivu.
Akizungumza
na waumini wa dini ya Kiislamu alipohudhuria sala ya Ijumaa leo (Julai
17, 2020) katika msikiti wa Buhari uliopo Ruangwa, mkoani Lindi, Waziri
Mkuu amesema ni muhimu Watanzania wakajenga tabia ya kuaminiana,
kuvumiliana pamoja na kupendana kwani mambo haya yote huchangia uwepo wa
amani na utulivu.
“Nchi
hii imejizolea sifa kuwa ni nchi ya amani na utulivu kwa sababu jambo
hili linahubiriwa na viongozi wa dini zote. Nchi hii sasa imekuwa ni
kimbilio la nchi ambazo zimepoteza amani kwenye nchi zao, wanakuja hapa
wanajifunza na wakirudi kwao wanaendelea kuwa salama,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuzingatia mahubiri ya
viongozi wa dini ili nchi iendelee kuwa na amani kwani kukiwa na amani
na utulivu lazima maendeleo yataonekana.
“Nchi
yetu imekuwa na kasi ya maendeleo katika maeneo mengi. Mimi naamini
maendeleo haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na amani tuliyonayo na hii
inatokana na mahubiri ya viongozi wetu wa dini. Dini ina mchango mkubwa
sana katika uendeshaji wa Serikali,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika Sala
ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Buhari , Ruangwa, Julai 17, 2020. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment