Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Benard Membe, akikabidhiwa fomu za ugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu Mkuu, Ado Shaibu.
Na Janeth Jovin
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya nje katika Serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha ACT-Wazalendo kimpitishe ili awanie urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
Membe amechukua fomu hizo leo Ijumaa mchana tarehe 17 Julai 2020 katika Ofisi za ACT-Wazalendo zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu.
Shaibu amesema, Membe alifanya mazungumzo na ofisi ya katibu mkuu akieleza adhima yake ya kwenda kugombea urais wa Tanzania na mchakato wa ndani bado unaendelea.
Amesema mchakato huo umeanza tarehe 1 Julai 2020 na bado unaendelea huku akisema wajibu wake kama katibu mkuu ni kumkabidhi fomu.
Baada ya kukabidhiwa fomu, Membe aliyewahi kuwa mbunge wa Mtama Mkoa wa Lindi akiwa na nyuso ya furaha wakati wote amesema, “napenda kutoa shukurani kwa ukaribisho mzuri alioupata ofisini kwake na kubwa lililonileta ni kuja kuitikia ombi la wanachama wa ACT-Wazalendo na Maalim Seif Sharif Hamad la kugombea urais.
“NImekabidhi ombi hilo kwa maandishi na nimekabidhiwa fomu ambazo nitakwenda kuzisoma na nitatekeleza vizuri sana, nitajaza vizuri sana, kwenye herufi kubwa nitaweka herufi kubwa,” amesema
Membe amesema, mpaka anachukua alikuwa peke yake na kutoa wito kwa wengine kwenda kuchukua fomu zipo nyingi “si kama wale wengine”
Amesema leo hana la kuongea zaidi, “siku nikirejesha fomu hizi nitakuwa na la kusema, nitamwaga cheche moja mbili tatu.”

No comments:
Post a Comment