HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2020

NHIF YASAJILI WANACHAMA WAPYA SABASABA

Na Tatu Mohamed

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao lililopo katika viwanja vya Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ili waweze kupata elimu pamoja na kujiunga na huduma hiyo.

Wito huo umetolewa na Ofisa Mkuu wa Masoko na Huduma za Wateja kutoka NHIF, Luhende Singu, ambapo amesema katika viwanja hivyo pamoja na kutoa elimu pia wanasajili wanachama wapya.

"Hivyo nitoe wito kwa wananchi na watanzania wote kwa ujumla kutembelea banda letu na kujiunga katika vifurushi vya bima kwani bima ya afya ni kinga dhidi ya janga la maradhi.

"Kimsingi nataka kuwaambia wataanza kuwa Bima ya afya sio unafuu wa matibabu au unafuu wa gharama za matibabu baada ya mtu kuanza kuugua bali bima ya afya ni kinga dhidi ya janga la maradhi, amesema Singu.

Amesema kila mwanachi anapaswa kuwa na bima kabla ya kuanza kuungua ili kuweza kuepuka gharama kubwa za matibabu bila ya bima.

"Mtu anapaswa kukata bima kabla hajaanza kuungua inatokea mara nyingi mtu anakwenda hospitali akishaona gharama zinakuwa kubwa ndipo anakwenda kutafuta bima hapo anakuwa atafuti bima bali anatafuta unafuu wa matibabu," amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages