Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi, Anthony Sanga (mwenye Shati
lenye Maya) akiangalia ramani ya mtandao wa mradi wa maji wa Ismani -
Kilolo wakati alipotembelea kukagua miradi mbalimbali ya maji mkoa wa
Iringa inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano. (Picha na Denis
Mlowe)
Na Denis Mlowe, Iringa
ZAIDI
ya wakazi 58,821 wa eneo la Mradi wa Maji Ismani -Kilolo wanatarajia
kunufaika pindi mradi wa Tanki kubwa unaojengwa na Mamlaka ya majisafi
na usafi wa Mazingira mkoa wa Iringa (Iruwasa) kwa kushirikiana na
Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) pindi
ukikamilika.
Mradi
huo ambao unatumia fedha za ndani kiasi Cha sh. Bilioni 9.27 ukiwa na
lengo la kuwaondolea changamoto ya maji wakazi wa vijiji 29 vitanufaika
katika mradi huo ambapo vijiji 5 vya Kilolo na vijiji 24 vya Ismani
vitapata maji Safi na Salama.
Akizungumzia
mradi huo Meneja Ufundi,Injinia wa Iruwasa,Fabian Maganga mbele ya
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga alipofanya ziara
ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano
chini jemedari John Magufuli.
Mhandisi
Maganga alisema kuwa mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa njia ya
force akaunti utatatua changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa
vijiji hivyo ukiwa una uwezo wa kuzalisha lita milioni 4.1 kwa siku
wakati uzalishaji ni 2.9 kwa siku kipindi Cha masika.
Alisema
kuwa mahitaji ya maji yanatarajiwa kufikia wastani wa Lita milioni 4
.65 kwa siku ifikapo mwaka 2038 hivyo mradi huu utakuwa suluhisho kubwa
kwa wakazi wa vijiji hivyo pindi ukikamilika.
"Mradi
huu wa maji wa Isimani -Kilolo utahudumia wakazi wengi na tunaamiji
itamaliza tatizo la maji kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi watapata
maji na kuondokana na kutembea mwendo mrefu kufuata maji"
Aliongeza
kuwa mtandao wa maji una jumla ya km 157 na unatoa Huduma kwenye
vitongoji 25 kwa Sasa ukiwa na matenki 25 yenye ujazo wa Lita 25,000
Hadi 150,000 ambapo hutolewa kupitia vituo 234 na muunganisho ya ndani
768.
Alisema
kuwa mradi huo ambao umeanza rasmi April 15 unatarajiwa kukamilika Juni
30 2021 ambapo wizara ya maji imekwisha toa milioni 450 kwa ajili
kuendeleza na ujenzi.
Kwa
upande wake, Meneja wa Ruwasa mkoa wa Iringa mhandisi ,Shaban Jellan
alisema kuwa mkoa wa Iringa unakabiliwa changamoto mbalimbali zikiwemo
uhaba wa vitendea kazi Kama magari kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji
wa miradi ambapo mahitaji ni magari 12 yaliyopo ni 5.
Alisema
kuwa changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi kwa ajili ya
usimamizi na uendeshaji wa miradi ambapo mahitaji halisi ya mkoa ni
wahandisi 18 waliopo ni 14 mafundi sanifu mahitaji ni 33 waliopo ni 11.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mhandisi, Anthony Sanga alitoa wiki 6
kwa Iruwasa na Ruwasa kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa njia
mbadala wakati mradi wa maji Ismani - Kilolo unamalizika na kuanza
kufanya kazi mara moja.
Aidha
akitoa wiki nne kwa Mamlaka hizo kuhakikisha wananchi wa Pawaga
wanapata maji Safi na Salama kutokana na mradi wa maji wa Pawaga
kukamilika kwa asilimia 90 hivyo waache maji yatoke wakati mradi
unakamilika ndani ya muda huo tofauti na muda wa miezi miwili waliotaka
mhandisi wa Ruwasa.
"
Mradi wa Maji wa Ismani - Kilolo Natoa wiki sita watu waanze kupata
maji kwa njia mbadala wakati mradi huu unaendelea kujengwa kuliko
kusubiri mradi ukamilike wakati wananchi wanapata tabu ya maji na natoa
wiki nne kwa mradi wa maji wa Pawaga ukamilike na watu wapate maji"Alisema.
Alisema
kuwa mradi huo uanze kujengwa haraka iwezekanavyo huku wizara inatoa
fedha nyingine kiasi Cha milioni 200 zitaingia Jumatatu ijayo na watu
waanze kuchimba mitaro kwa ajili ya kuendelea na mradi.
Alisema
kuwa vibarua watumike wazawa wa maeneo husika kwani inasaidia kuongeza
ajira kwa wananchi ikiwa ni lengo la Rais Magufuli kuwaletea maendeleo
na kuongeza ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment