HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2020

MGOGORO WA ARDHI SHULE YA MSINGI BOHALI WAZIDI KUFUKUTA



NA LYDIA LUGAKILA, KARAGWE


Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, ameazimia kumaliza mgogoro wa ardhi wa kiwanja cha Shule ya Msingi Bohali iliyopo kata Bugene wilayani Karagwe Mkoani Kagera uliodumu kuanzia mwaka 2003 hadi sasa kati ya mwekezaji binafsi baada ya kuendelea kufukuta licha ya shule hiyo kushinda kesi mahakamani.


Hayo yamejiri katika mahafali ya 8 ya shule ya msingi bohali iliyopo wilayani Karagwe Mkoani Kagera katika lisala ya shule iliyosomwa na mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Bwana Ananias Kishenyi mbele ya wazazi na mgeni rasmi iliyoeleza kuendelea kufukuta kwa mgogoro wa kiwanja cha eneo la shule jambo ambalo limeonekana kukwamisha maendeleo ya shule hiyo.


Kishenyi amesma kuwa kuwa vyombo vya sheria hususani Mahakama vimeweza kutekeleza vyema wajibu wake jambo lililowafanya kufanikiwa kushinda kesi hiyo na kuwa hadi sasa bado mgogoro huo umefukuta tena huku akiiomba serikali kuingilia kati ili shule hiyo itoe huduma kwa watoto bila vikwazo.


Akijibu lisala hiyo mgeni rasmi katika mahafali hayo, IVO Emmanuel, mwakilishi wa mbunge wa jimbo la karagwe na waziri wa viwanda na biashara, Inncent Bashungwa kwa njia ya simu amesema kuwa eneo hilo ni muhimu kwa ajili ya kutoa taaluma kwa watoto hivyo yupo tayari kuanzia sasa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa serikali ili kuona namna nzuri ya kumaliza mgogoro huo.


Mahafali hayo ya 8 ya shule ya bohali yameunganishwa na mahafali ya pili ya shule ya sekondari St. sesilia iliyoko halmashauri ya wilaya ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment

Pages