HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2021

DIWANI KATA YA TANGINI AWEKA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UCHAFU WA MAZINGIRA


Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kalanguti aakiwa katika zahanati alipotemnbelea na kufanya ziara kwa ajili ya kuweza kujionea shughuli mbali zinazofanywa pamoja na suala zima la utunzaji wa mazingira sambamba na usafi katika maeneo ya kazi. (Picha na Victor Masangu).

 

 

NA  VICTOR MASANGU, PWANI 

 

KATIKA kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu katika suala zima la  kupambana na usafi wa mazingira Diwani wa kata ya Tangini Mfalme Kalanguti kupitia tiketi ya (CCM) ameahidi kuanzisha kampeni maalumu kwa kushirikiana na wananchi wake yenye lengo la kuendesha zoezi la kufanya usafi  nyumba kwa nyumba kila mwishoni wa juma ili kuthibiti kuibuka kwa magonjwa mbali mbali ya milipuko.

Kalanguti aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea katika kuhakikisha anapambana vilivyo ili kuweza kuwasaidia wananchi waweze kuondikokana kabisa na magoinjwa mbali mbali ya mlipuko amabyo  yanaweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa kuzagaa kwa uchafu katika maeneo ya makazi ya watu.

“Kwa upande wangu mimi kama Diwani wa kata ya Tangini pamoja na kuweka mipngo madhubuti ya kushirikiana na wananchi wangu katika masuala mbali mbali ya kimaendelea lakini moja katika ya mipango yangu ni kuunga juhudi za serikali katika suala la mambo ya usafi wa mazingira hivyo mimi zoezi langu nitakalolianzisha litakuwa endelevu na kwamba litakuwa likifanyika kila mwisho wa  wiki ambapo kila mwananchi ataweza kushiriki kikamilifu lengo ikiwa ni kutbitibinna kupambana na magonjwa ya milipuko,”alibainisha Kalanguti.

Pia Diwani huyo alisema kuwa pamoja na kuendesha kampeni hiyo pia atashirikiana bega kwa began a wataalamu mbali mbali wa masuala ya afya ili kuweza kutoa elimu zaidi kwa wananchi wake kuhusina na umuhimu wa kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo ambayo wanayoishi hasa katika kipindi cha mvua zinapokuwa zinanyesha.

“Suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo wananchi wanapaswa kuliangalia kwa jicho la tatzu zaidi na kushiriki kikamilifu bila ya kutegea kwani  magonjwa ya milipuko yanatokana na kuwepo kwa kuzagaa kwa uchafu mbali mbali hivyo nina imani tukishiriki kikamilifu kwa pampoja tutaweza kukabiliana na hali hii ya magonjwa ya milipuko.,”aliongeza Kalanguti.

Pia aliongeza kuwa katika kukabiliana na wimbi la magonjwa mbali mbali ya mlipuko wananchi wote wanapashwa kuendesha shugghuli zao kwa kuzingatia sheria za na taratibu ambazo zimewekwa na kuheshimi miongozo yote ambayo inatlewa na wataalamu wa afya lengo ikiwa ni kuweza mazingira yawe katika hali ya usafi.

Kalanguti pia aliweza kuiasa jamii kwa ujumla kujenga tabia ambayo ni endelevu ya kuhakikisha kwamba wananawa mikono yao kwa kutumia maji  safi na salama ambayo ni tiririka ili kusaidia kupambana na magonjwa hayo ya mlipuko na kutoa pongezi kwa serikali ya wamu ya tano kuweza kuwahamasiha wananchi katika suala zima la kufanya usafi katika kila mwisho wa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Pages