HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2021

RAIS MAGUFULI KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO-KAGERA

 Na Lydia Lugakila, Bukoba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekaji mawe ya msingi katika miradi mkoani Kagera.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kagera na  waandishi wa habari  juu ya ujio wa Rais Dk. John Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco, Gaguti amesema ziara hiyo itaanza Januari 18, 2021 ambapo Rais Magufuli atafanya matukio yatakayohusisha uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa chuo cha ufundi Veta mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 22, uzinduzi wa shule ya sekondari ya Ihungo wenye thamani ya shilingi takribani bilioni 11.1.


Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa licha ya shughuli hizo Rais Magufuli atapata fulsa ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa uchimbaji wa madini aina ya Nikel ambapo pia atatembelea na kujionea  ufugaji wa kisasa mradi ambao ukikamilika utakuwa na thamani ya shilingi bilioni 15.

Aidha kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa pia Rais Magufuli atawahutubia wananchi Mkoani humo katika uwanja vya michezo wa shule ya sekondari Ihungo na baadae ataelekea wilayani Karagwe Mkoani humo kwa ajili ya kutembelea na kuweke jiwe la msingi katika mradi wa ufugaji wa kisasa ambao utaishia kuwa na kiwanda Cha kisasa Cha maziwa.

Hata hivyo Brigedia Gaguti ametumia fulsa hiyo kuwataka wananchi Mkoani Kagera kujitokeza kwa wingi ili kumpokea kiongozi huyo

No comments:

Post a Comment

Pages