HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 09, 2021

Dk.Jingu : Wasajili wa NG'Os fanyeni kazi kwa maslahi ya nchi

KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John Jingu, akifafanua jambo.

Na Asha Mwakyonde


KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu, amewataka Wasajili wa Wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S), kufanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Dk. Jingu ameyasema hayo leo kupitia UFM wakati akizungumza mafunzo ya Wasajili Wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S), ambayo yameanza juzi  kwa ngazi ya mikoa na Halmashauri yanayotarajiwa kufanyika nzima.

Dk. Jingu amesema mafunzo hayo yana lengo kubwa la kuwafanya wasajili hao  wayajue majukumu yao.

Amesema kilichowasukuma kufanya mafunzo hayo ni kwamba maofisa hao wengi ni wapya ambao wamepewa majukumu siku za hivi karibuni.

KATIBU huyo ameongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida maofisa hao wakishakabudhiwa majukumu yao  lazima waeleweshwe, wapewe ufahamu  wa nini wanatakiwa kufanya na mipaka ya majukumu yao.

"Kiufupi wanatarajiwa wao Kama maofisa wa Serikali waliopewa jukumu la kuratibu shughuli za mashirika hayo katika maeneo yao mikoani,kwenye  Halmashauri, Wilaya wanatakiwa wafanye kazi zao kwa uadilifu, uwajibikaji kazi , kujitoa  kwa kuzingatia maslahi ya Taifa," amesema Dk. Jingu.

Amesema maofisa hao wameteuliwa hivi karibuni lakini wanafanya kazi vizuri, wanaelewa sheria inataka nini, kanuni ya GN ya 687  inaeleza vizuri majukumu yao.

Dk. Jingu ameeleza kuwa mafunzo hayo wamezungumza mambo mengi likiwamo la kusimamia sheria.

Amesema sheria inalazimisha Mashirika hayo kufanya kazi kulingana na katiba ambazo wamesajili nazo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages