HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2021

FOMMA KUSHUSHA NEEMA KWA MAKUNDI YA WAHITAJI

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA


JAMII imeshauriwa kuwekeza kwa watu wenye shida mbalimbali,ikiwemo wajane,yatima,wazee na wasiojiweza badala ya kuwekeza kwenye starehe na hanasa.


Ushauri huo umetolewa leo 17 Januari 2021 na mwanzirishi wa umoja wa kuwasaidia wajane,yatima,wazee na makundi ya watu wasiojiweza Mc John Mwangata ujulikanao kama Friends of Mc Mwangata Association(FOMMA) wakati wa afla ya kutimiza mwaka mmoja iliyofanyik Msalato Jijini Dodoma.


Mc Mwangata akizungumza mbele ya wanachama wa umoja huo amesema kuwa ili kuweza kuwa na taifa la watu wenye furaha na upendo ni vyema wale wenye kujariwa kuwa na uwezo kujenga tamaduni ya kuwakumbuka ambao ni wahitaji.


"Watanzania Mungu katijalia kwa kiasi kibubwa cha kuonesha upendo kati ya mtu na mtu, lakini tujue kuwa hatulingani kwa kipato wapo watu ambao wanauhitaji mkubwa na kwa kulitambua hilo ni vyema kuwakumbuka watu wa aina hiyo.


"Na kutoa kwa wahotaji siyo jambo baya wapo watu wanatumia mali zao kwa kustarehe na kufanya anasa za kutisha lakini wanawasahau watu wenye uhitaji,sasa kwa kuliona hilo ndugu zangu naombeni tuwekeze kwa kada ya watu Wa aina hiyo na hakika Mingu atatuongezea na tutaongeza furaha na maisha marefu kwa watu wa aina hiyo"amesema Mc Mwangata.


Katibu wa Umoja huo Godbless Kisanga,akisoma Risala amesema Umoja huo( FOMMA) ulioanzishwa mwaka 2019 na umejipanga katika mwaka 2021 kuhakikisha wanawafikia watu wenye uhitaji ndani ya mkoa wa Dodoma na nje ya Dodoma kwa kutoa huduma mbalimbali kwa watu wenye wahitaji.


Kisanga amewasilisha risala hiyo wakati wa  tafrija fupi ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa umoja huo ujulikanao kama (FOMMA).


Kisanga amesema kuwa Mc Mwangata alianzisha umoja huo kwa maono ya kuwasaidia watu wenye uhitahi sambamba na kuwatembelea na kuwasaidia waliopo magerezani.


Kisanga ambaye ni Katibu katika Umoja huo amesema lengo la umoja huu ni kufahamina, kusaidia wasio jiweza na kusaidiana wao Kwa wao huku  lengo kuu likiwa zaidi ni kuwasaidia yatima,wajane,wazee pamoja na wale waishio katika maisha magumu.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja huo Dk.Gaspaer Kisenga,amesema umoja huo umeanzishwa mahususi kwa lengo la kuwafanya watu wasiokuwa na uwezo nao kujiona hawajasahaulika katika Jami.


"Mimi kitaaluma ni Daktari katika kituo cha Afya Makole ninaona jinsi watu wanaohitaji huduma wanavyotesema na wengine hata kupata matibabu inakuwa shida.


"Kwa kuliona hilo kikundi chetu ambacho mwanzilishi ni Mc Mwangata tuliona jambo muhimu zaidi ni kujikita katika kuwasaidia wahitaji ambao wapo katika makundi ya wajane,yatima,wazee na wanaoishi katika mazingira magumu"amesema Dk.Kisenga.

No comments:

Post a Comment

Pages