Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama, akizungumza jambo na baadhi ya watumishi wa serikali pamoja na waandishi wa habari kuhusiana na masuala mabalimbali ya kuweka mikakati ya kuleta maendeleo.
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha usafi wa mazingira na kudhibiti kutokea kwa amlipuko wa magonjwa mbalimbali imeamua kuweka sheria ndogondogo zitakazotumia kuwachukulia hatua kali wananchi watakaobainika kutupa uchafu ovyo ambao unaweza kuhatarisha usalama wa afya zao ikiwemo kuwapiga faini ya kuanzia kiasi cha shilingi laki mbili na kuendelea.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama, wakati akizungumzia kuhusiana na mikakati endelevu waliyoiweka katika kutekeleza azma ya agizo la Makamu wa Rais la Mama Samia Suluhu la wananchi wote kufanya usafi katika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kwamba itaweza kuwasaidia wananchi kuondokana na ile hali ya kupata magonjwa ya mlipuko.
Gama alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaweka misingi imara kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbai ikiwemo katika masoko, zahanati, hospitali pamoja na sehemu za barabarani.
“sisi kama halmashauri ya Kisarawe hatuna mzaa kabisa katika suala zima la usafi wa mazingira na hii ni hatua ya utekelezagi wa maaagizo ambayo yalitolewa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kuhakikisha kwamba wananchi wote wanafanya usafi katika maeneo yao ya makazi nay ale ya biashara katika kila juma mosi ya mwisho wa mwezi na sisi ili tunalifanya kazi ipasavyo bila masihala,”alisema Gama.
Aidha Gama katika kutimiza azma hiyo ya serikali ya awamu ya tano katika kuwathibiti baaaadhi ya watu ambao wamekuwa wakienda kinyume cha sheria na taratibu ambazo zimewekwa tayari wameshaweka sheria kali kwa kushirikiana na baraza la madiwani ambazo zitatumika katika kuwawajibisha wale wote ambao watabainika wanachafua mazingira kwa makusudi.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kwa sasa katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawewananchi walio wengine tayari wameshaanza kuyazingatia maelekezo mbali mbali ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya kuhusiana na madhara ya utupaji wa taka ovyo yanaweza kusababisha kutokea kwa milipuko ya magonjwa mbali mbali.
Katika hatua nyingine Gama hakusita kuwaasa wananchi wote wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha kwamba wanaendelea kuzingatia misingi ya kulinda afya zao kwa kuendelea kunawa mikono yao kwa kutumia maji tiririka na sabuni wakati wa kula vyakula kwa lengo la kuthibiti hali ya kutokea kwa magonjwa ya aina mabli mbali kama vile kuhala pamoja na kuumwa na matumbo.
No comments:
Post a Comment