Na Talib Ussi, Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar wameshauriwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia Damu ili kuokoa maisha ya watu.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Ngome ya Wanawake Chama cha ACT Wazalendo, Janet Fussi wakati alipoungana na viongozi Pamoja na wanachama wa Ngome hiyo kuchangia damu katika kituo cha Damu Salama kiliopo kwa wazee Sebleni Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema hivi sasa mahitaji ya damu ni makubwa katika hospital za Zanzibar hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kuchangia damu ili iwe sababu ya kuhami maisha ya wenzao ambao wanahitaji damu.
Alisema hakuna ambaye atawaletea damu kama wazanzibar wenyewe hawajachangia Damu.
Aliwaomba wale wote ambao wanaafya njema hasa Vijana kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara ili hospitali za zanzibar ziwe na damu ya kutosha.
Aliwataka watu kuacha kuwa na ghofu katika kufanya jambo alililoita jema hasa kiimani kwa kile alichosema kuwa unapookowa maisha ya mtuu na kwa mwenyezi unapata fungu kubwa.
Alisema wahitaji wakubwa wa damu ni wanawake na Watoto kwa hiyo kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha maisha yao yanakuwa salama kwa kujitolea kuchangia damu.
Kwa upande wake Daktari Mkuu wa kituo cha Damu Salama Bakar Hamad Magarawa alisema kipindi hiki kuna mapungufu makubwa ya damu na kuwaomba wananchi wengine waige Ngome ya Wanawake wa ACT wazalendo ili kuondoa upungufu huo.
Alisema asilimia 70 ya wahitaji wa damu ni wanawake wajawazito Pamoja na wale wenye ugonjwa wa matumbo na kueleza kuwa watu wakijitokeza kuchangia damu basi inaweza kuwahami akina mama na wahitaji wengine.
“Natoa wito kwa wazanzibar wote tujitokeze kwa wingi kuchangia damu kwani Chupa moja ya Damu ni sawa na kuokowa maisha ya watu watatu” alisema Magarawa.
Alisema kituo hicho hakiwezi kuwa na damu kama wananchi hawajahamasika kuchangia damu.
“Changia Damu kwa kuokoa maisha ya watu” alisema Magarawa.
Attiye Ali Salim mwenyekiti wa Ngome hiyo mkoa wa Mjini Kichama alisema anajisikia furaha kuwa miongoni mwa wale waliochangia damu kwa ajili ya ustawi afya wa Zanzibar wanahitaji damu.
Alisema unapochangia damu hata mwenyewe anaweza kuja kuitumia mara akipata maradhi ya kuongezewa damu.
“Tusione kama tunachangia watu tuu hata sisi wenyewe inaweza ikatumika” alisema Attiye.
Rais Abdallah Mussa mwenyekiti wa Ngeme hiyo Wilaya ya Magharibi A alisema nchi yoyote haiwezi kuwa na maendeleo kama wananchi wake hawana afya njema kwa hiyo kuchangia damu sehemu kuchochea maendelea ya nchi.
“Na sisi kama wanachama wa ACT Wazalendo tunawajibu wa kuisaidia Serikali yetu ka juhudi za kufikia maendeleo kwa kusaidi kutoa damu kwa ajili kustawisha afya za wengine” alisema Bi Raisa.
Alisema havi sasa Viongozi wakuu wa Serikali wako kitu kimoja katika kuhakikisha maendeleo ya Zanzibar yanakuwa kwa haraka hakuna na wananchi wake kuwa kitu kimoja kwa kusaidia shida mbali mbali ikiwe Damu.
Sambamba na hilo Bi Raisa aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwajenga wananchi wao kuwa na moyo wa kujitolea kwa kila jambo hasa hilo la kuokowa maisha ya watu.
Viongozi hao Ngome ya Wanawake Miko ana Taifa wameshiriki tukio la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment