Lydia Lugakila, Muleba
Jumla ya mahabusu 126 kutoka Wilaya ya Biharamulo, Muleba na Bukoba mkoani Kagera wamefutiwa mashitaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili na Mkurugenzi wa Mashitaka hapa nchini DPP.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Muleba Mkurugenzi wa Mashitaka hapa nchini, Biswalo Mganga, amesema kuwa waliofutiwa mashitaka hayo kwa wilaya ya Muleba ni 26, Bukoba 52 na Biharamulo ni 48 na wote walikuwa na makosa mbalimbali.
Mganga amesema kuwa sababu iliyosababisha kuwepo kwa maabusu hao ni wao kwa wao kubambikiziana kesi, migogoro ya ardhi, wivu wa kimapenzi pamoja na migogoro ya kifamilia ambapo amewataka Wananchi Mkoani humo kutatua migogoro yao ngazi ya serikali za vijiji badala ya kwenda ngazi ya Mahakama.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ameshukuru Mkurugenzi huyo DPP kwa kufuta mashitaka hayo ambapo Wilaya ya Muleba ilikuwa na maabusu 126 na kufanya kupunguzwa na kubaki 100 katika gereza la wilaya Muleba.
January 17, 2021
Home
Unlabelled
MAHABUSU 126 WAFUTIWA MASHTAKA MKOANI KAGERA
MAHABUSU 126 WAFUTIWA MASHTAKA MKOANI KAGERA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment