HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 31, 2021

Takukuru yatambua mchango wa Habari Mseto Blog katika mapambano dhidi ya Rushwa


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Habari Mseto Blog, John Dande, kwa kutambua mchango wake katika mapambana dhidi ya rushwa.

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imetambua mchango wa blog ya Habari Mseto Blog katika kufanikisha  mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini.

Takukuru imetambua mchango huo leo Januari 28,2021 wakati wa utoaji vyeti vya pongezi kwa vyombo mbalimbali vya habari na Habari Mseto Blog ikiwemo, tukio lililokwenda sambamba na uzinduzi wa chaneli mpya ya TAKUKURU TV ya YouTube.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa anatambua mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya rushwa.

Amesema kutokana na kutambua mchango huo wa waandishi wa habari ndio maana wamevitunuku vyombo mbalimbali vyeti vya pongezi kama ishara ya kuthamini na kutambua mchango wao katika mapambano hayo ya rushwa.

"Hakuna asiyetambua kuwa kalamu ya mwandishi wa habari ina nguvu kuliko Upanga, hivyo basi ni muhimu mkatumia vizuri kalamu zenu kwani tunatambua kuwa zina nguvu katika kushawishi na kuchochea watu kufanya kazi za Maendeleo," amesema Brigedia Mbungo.

Naye Mkurugenzi wa Elimu kwa umma Takukuru makao makuu, Joseph Mwaiswelo amesema kuwa vyombo vya habari ni nyenzo thabiti na Kiungo muhimu kati ya Taasisi ya Takukuru na wananchi  hivyo wataendelea kushirikiana navyo.

Aidha amesema Taasisi hiyo kwa sasa imeanzisha TV yake ya YouTube na kuongeza kuwa kupitia Televisheni hiyo wananchi wataweza kupata habari mbalimbali zinazohusiana na mapambano dhidi ya rushwa.

No comments:

Post a Comment

Pages