Na Asha Mwakyonde
DIWANI wa Kata ya Tandale iliyopo Wilaya ya Kinondoni Chifu Abdallah Saidi wanatarajiwa kuandaa mashindano yenye lengo la kukuza vipaji vya vijana wa kata hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2021 Chifu Saidi amesema michezo ni ajira kwa vijana wenye vipaji na wanaojituma kwa kile wanacho kifanya.
Diwani huyo amefafanua kuwa mashindano hayo yatahusisha mpira, Pet, rede na mingine ikiwa ni pamoja na ngumi.
" Niliahidi kutengeneza nyumba ya kukuza vipaji vya vijana wa Tandale ( House of Talent), ili vijana hao waweze kupata ujuzi zaidi," amesema Chifu Saidi.
Amesema mbali na kujitenenezea ajira vijana hao kupitia michezo pia wataweka afya zao katika hali nzuri kutokana na michezo hiyo.
Diwani huyo ameongeza kuwa vijana wapo vijana ambao wamejituma kwa kucheza kwa bidii katika mchezo anaoupenda na kufanikiwa katika maisha yao na kuzisaidia familia zao kiuchumi.
Chifu Saidi ametolea mfano kwa mchezaji Mbana Samatta ambaye amepata mafanikio makibwa ya kucheza nje ya nchi na kuitambulisha Tanzania vema.
Amewataka vijana wa Kata ya Tandale kujitokeza kwa wingi mashindano hayo yatakapoanza ili waonyeshe vipaji vyao na baadae waweze kusaidiwa.
No comments:
Post a Comment