HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 21, 2021

Mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara anauwezo mkubwa wa kusambaza Virusi vya HPV

Na Asha Mwakyonde

DAKTARI wa Magonjwa ya Binadamu kutoka Hospitali ya Marie Stopes, Mwenge , Dkt. Mashingo Lerise amesema kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara kunaweza kusababisha mwanamke kupata Saratani ya mlango.was kizazi kutokana na maambukizi ya aina ya virusi vijulikqnavyo kama Human Papilloma Virus (HPV)

Amesema  maambukizi ya kirusi  kinachojulikana kama (HPV), husababisha saratani ya mlango wa shingo ya kizazi._

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaama jana daktari huyo amesema kuwa mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara anauwezo mkubwa wa kusambaza virusi vya HPV pamoja na maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa.

"Kutofanya tohara kwa mwanaume kuna tengeneza mazingira rafiki ya kuvisambaza Virusi hivyo ambavyo vinapatikana zaidi kwenye maji maji ya kwenye viungo vya uzazi " anesema Dkt. Lerise.

Ameeleza kuwa serikali na taasisi mbalimbali imekuwa ikipiga kelele ili wanaume ambao hajawatahiriwa wafanyiwe tohara kwa lengo la kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na Virusi hivyo ambavyo husababisha saratani ya shingo ya mlango wa Kizazi.

Daktari huyo amesema kuna vihatarishi vingine vinavyomuweka mtu kwenye hatari ya kupata saratani ya mlago wa shingo ya  kizazi ikiwa ni pamoja na kuanza vitendo vya ngono mapema, mimba chini ya umri wa miaka 16, kuwa na mahusiano na wanaume wengi na historia ya ugonjwa huu kwenye familia.
 
Pia kuwa na idadi kubwa ya watoto, kuzaa mara kwa mara, umri zaidi ya miaka 30 na  mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye mwenza wake amefariki kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi..

Ugonjwa wa  saratani una aina zaidi ya 200 tofauti kutegemeana na kiungo kilicho athirika kama vile seratani ya matiti,mlango wa uzazi, tezi dume, koo, damu na nyingine.

No comments:

Post a Comment

Pages