HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 21, 2021

TTCL CORPORATION YAANZA NA WABUNGE

 

Mhe. Humphrey Polepole (mwenye tai), akipatiwa maelezo na Meneja Mahusiano TTCL, Bi. Puyo Nzalayaimisi juu ya vifurushi vinavyotolewa na TTCL CORPORATION alipotembelea viwanja vya Bunge leo asubuhi.

 

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, Mb (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya kalenda ya mwaka 2021 na Meneja Mahusiano wa TTCL Bi. Puyo Nzalayaimisi (Kulia) mapema leo asubuhi katika viwanja vya Bunge.

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile (katikati), akifafanua jambo kwa watoa huduma wa TTCL waliotembelea viwanja vya Bunge mapema leo.

 

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

 

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION), limeanza kutekeleza baadhi ya maagizo ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Baadhi ya maagizo yaliyotolewa na Mhe. Ndugulile alipozungumza katika kikao kazi cha Shirika hilo kilichojumuisha viongozi wa Shirika na Mameneja wa Mikoa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma. Miongoni mwa maagizo yaliyotolewa ni pamoja na Shirika kuendelea kujitangaza, kuboresha bidhaa, kuboresha huduma kwa wateja  na kuongeza ubunifu.

Katika utekelezaji huo, baadhi ya watumishi wa Shirika hilo wakiongozwa na Meneja wa Mahusiano Bi.Puyo Nzalayaimisi, wameanza utekelezaji wa maagizo hayo katika viwanja vya Bunge kwa kutangaza zaidi bidhaa zao kwa kipindi chote cha Bunge. Huduma zinazotolewa kwa Waheshimiwa Wabunge ni pamoja na Usajili wa laini za TTCL, Huduma za T-PESA na Uuzaji wa bidhaa zinazotolewa na Shirika hilo.

Mmoja wa wabunge waliohudumiwa ni Waziri wa Afya na maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) ambaye alilitaka Shirika kuendelea kutoa na kuboresha huduma ya mawasiliano katika sekta ya Afya Nchini.

Naye Meneja wa Mawasiliano wa Shirika hilo Bi. Puyo Nzalayaimisi aliahidi kuendelea kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Mawasiliano, “Kama Shirika la Mawasiliano Nchini tutaendelea kutoa huduma zetu zenye viwango bora na kulitangaza Shirika letu ili kufikia malengo pamoja na kutimiza maazimio yaliyotokana na kikao kilichopita” alisema Bi.Puyo.

No comments:

Post a Comment

Pages