Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Maelekezo ya Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kuhusu utoaji wa habari za Serikali kwa umma
yanatekelezwa kwa kasi na ofisi au mtendaji yeyote wa ofisi ya umma
atakayekaidi asitafute wa kumlaumu.
"Waziri wa
Habari Mhe Innocent Bashungwa, hivi ninavyoongea hapa ameshasaini barua
yenye maelekezo hayo na zaidi kuzijulisha taasisi zote za umma nchini
kuhusu tathmini itakayofanyika," alisema.
Dkt.
Abbasi ameyasema hayo leo mkoani Morogoro wakati akitoa mada kwenye
semina ya wahariri kuhusu Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius
Nyerere.
Amesema utoaji wa habari kwa umma ni
jambo la kisheria na kikatiba hivyo hata maelekezo ya Rais yako sahihi
na atakayekaidi "amekaidi mamlaka, amekaidi sheria na amekaidi katiba."
Katika
hatua nyingine, Dkt. Abbasi amewataka wahariri na waandishi nchini
kuenzi misingi ya weledi na uzalendo katika kazi zao ikiwemo kufanya
utafiti kwanza kuliko "kufakamia" mawazo na maoni ya watu wasioitakia
nchi mema.
"Baadhi ya waandishi hawafanyi
utafiti wala kutaka kujua mambo kwa kina na huishi wakifakamia tu kila
kinachosemwa na mabeberu kupinga maendeleo yetu. We mwandishi gani sisi
ndio Serikali na ndio wenye hela na ndio wenye mradi tunakwambia
tunakwenda kujenga mradi Rufiji, anatokea wakala wa mabeberu mmoja
kashiba mivyakula ya kwenye kopo huko anakofadhiliwa kuishi anakwambia
huo mradi hautajengwa, hawana hela hao, mwandishi unatoka unamwamini
wakala wa beberu unaandika na kusambaza uongo, we vipi mbona hatukuelewi
na wewe ni wa moto au wa baridi?" alihoji Dkt. Abbasi akisisitiza tangu
utekelezaji wa mradi wa Umeme JNHPP Rufiji uanze hakuna malipo ambayo
Serikali imechelewesha au kushindwa kuwalipa wakandarasi.
No comments:
Post a Comment