HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2021

JKT, WIZARA YA KILIMO WASAINI MKATABA WA MARIDHIANO LENGO LIKIWA TAIFA LINAPATA CHAKULA CHA KUTOSHA

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali  Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya  wakitiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kilimo wakati wa  hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya JKT, Wilaya ya Chamwino, Dodoma. (Picha na Richard Mwaikenda).

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali  Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya wakibadilisha hati baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kilimo wakati wa  hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya JKT, Wilaya ya Chamwino, Dodoma. 

 

NA  HAMIDA RAMADHANI DODOMA


JESHI la Kujenga Taifa (JKT)  limetia saini mkataba wa maridhiano na Wizara ya Kilimo  lengo likiwa ni kuhakikisha wanashirikiana pamoja ili Taifa lipate chakula cha kutosha na kuepukana na majanga ya njaa.

Akizungumza  leo Jijini hapa Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja Generali Charles Mbuge amesema mashirikiano hayo yana lengo la kulinufaisha Taifa kwani Taifa likiwa na njaa  shughuli za kiuchumi haziwezi kufanyika.


Aidha Meja Generali Mbuge amesema kilimo ndio uti wa mgongo ambapo kwa Tanzania Kilimo kinahusisha matabaka yote  wenye kipato na wasio na kipato.

"Makubaliano hayo Kati ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) yamekuja wakati muafaka kwani vijana wengi wa Tanzania wamekua wakijitolea  kwenye mafunzo yetu ya JKT hivyo wakiwa ndani ya Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT) watapatiwa mafunzo ya Kilimo ambapo tunahakika na wao wataenda kuitumia vizuri pindi wawapo uraiani,".


Na kuongeza kuwa "Jeshi ni chombo pekee ndani ya Taifa letu hivyo endapo likitumiwa vizuri litaleta manufaa makubwa katika Taifa,"amesema Meja Generali Mbuge.

Hata hivyo amesema Jeshi la kujenga Taifa (JKT) imeshaanza shughuli za Kilimo kwa mazao ya kimkakati Katika maeneo mbalimbali ya hapa Nchini.

Naye Kanali Hassan Mabena ambae ni  Kaimu Mkuu wa Utawala JKT amesema lengo la kuwekeana saini ni kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kulipunguzia Taifa mzigo.

"Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limejiwekezea nguvu kubwa katika vikosi vyake kwani mazao yote ya kimkakati  yanalimwa Katika vikosi hivyo," Kanali Mabena.

Aidha amebainisha  changamoto wanazokumbana nazo katika Kilimo ni mabadiliko ya tabia nchi, na uhaba wa pembejeo za Kilimo.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema makubaliano hayo yalikua ni ndoto yake ya kila siku kwani yeye ni mfatiliaji mkubwa katika shughuli wanazo fanya Jeshi la kujenga Taifa (JKT).

kukutana kwao na kuekeana saini ni Kati ya moja wapo ya Malengo Makubwa aliyekuwa akiyawaza  kwani  Jeshi la kujenga Taifa (JKT) shughuli za kilimo wanazo fanya ni wazi zinajulikana ila wizara ya kilimo ndio vinara wa Kilimo Nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages