NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleimani Jafo, amezitaka Mamlaka za Maji nchini kuweka miundombinu ya maji kwa wingi ili iwe rahisi kwa Jeshi la Zimamoto kupata huduma ya maji pindi wananchi wanapokumbwa na majanga ya Moto.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini hapa kwenye uzinduzi wa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama cha Skauti Tanzania.
Waziri
Jafo amesema Jeshi la Zimamoto limekuwa likijitoa kufa na kupona katika
kuhakikisha tu, pale wananchi wanapopatwa na majanga ya moto wanasaidiwa
kwa weledi na wakati licha ya lawama nyingi kupata kutoka kwa wananchi.
"Leo
nimepata furaha Sana baada ya kuona kwamba miundombinu yetu hasa ya
shule inaenda kunusulika na kwa kufanya hivi tutapunguza kwa kiasi
kikubwa matukio ya majanga ya moto ya mara kwa mara mashuleni kwani
makubaliano haya hakika ni mafanikio makubwa ,".
Na
kuongeza "Huu ni mwanzo mpya kwani tunakwenda kusaidia Taifa letu hasa
katika miundombinu yetu ya shule bila kusahau serikali inamtumia
mabilioni ya Fedha kujenga na kukarabati shule na mwisho wa siku
kuteketea kwa moto," amesema Waziri Jafo.
Amesema
makubaliano hayo kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama cha Sikauti ni njia
bora kwani na wao watakwenda kuwafundisha Vijana wenzao huko mashuleni
mbinu za awali za kujikinga na majanga ya Moto.
Awali
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Khamis Hamza amesema kwa hivi karibuni
matukio ya Moto yamekithiri hali inayopelekea wengine kupoteza
maisha,kupata ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza mali zao.
"
Licha ya kuwepo kwa matukio hayo ya mara kwa mara jeshi la zimamoto
nchini limeendelea kuchukua hatua mbalimbali kama kujenga visima vya
Dharura,na kutoa elimu ya majanga ya moto kwa wananchi,"
Na
kuongeza "Na leo niseme tu ni jambo jema kwani mashirikiano Kati ya
Jeshi la Zimamoto na Chama cha Sikauti kwa kuwapa elimu ya kupambana na
majanga ya Moto kwa njia ya awali hakika tunakwenda kulidhibiti suala
hili," amesema Hamza
Kwa
Upande wake skauti Mkuu Mwantumu Mahiza amesema Skauti Tanzania
kwakutambua kwamba Serikali inamtumia gharama kubwa katika kujenga na
kukarabati shule na ndio maana wameridhia makubaliona hayo kati ya
Jeshi la Zimamoto na Chama cha Skauti Tanzania.
Aidha
amesema chama cha skaut kimekua kikijishughulisha katika majanga
ambavyo yamekuwa yakitokea nchini kusaidia na kuokoa uhai na mali za
wananchi.
"Hivyo basi
makubaliano haya kati ya Jeshi la Zimamoto na Chama cha Skauti ni
mafanikio makubwa katika kuhakikisha mali za shule zinanusurika na
majanga ya moto.
No comments:
Post a Comment