HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 05, 2021

KATIBU TAWALA WILAYA YA BAGAMOYO AIPIGIA CHAPUO TIMU YA BAGAFRIENDS MABINGWA WA DARAJA LA TATU


 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni (kulia), akizungumza na baaadhi ya viongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA) walioongozwa na Mwenyekiti wao Olnjilie Maliwa (kushoto) kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuisaidia timu ya Bagafriends ambao ndio mabingwa wa ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani.

 

  

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

 

Katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kukuza sekta ya michezo husaan mchezo wa soka  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni amewaomba wadau mbali mbali wa michezo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuisaidia kwa hali na mali  timu ya soka ya Baga friends ambayo ndio mabingwa wa ligi ya soka daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani ili ifanye vizuri katika hatua ya ligi ya mabingwa wa Mkoa ngazi ya  Taifa.

Mgeni ametoa rai hiyo wakati alipotembnelewa na  baadhi ya viongozi wa Chama cha soka Wilaya ya Bgamoyo (BFA) Ofisni kwake pamoja na kamati ya utendaji ya timu hiyo ya Bgafriends kwa ajili ya kuweza kuwek mikakati amabyo itawesa kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika hatua nyimgine inayofuata ya ngazi ya Taifa.

“Lengo la kukutana na viongozi hawa wa mpira wa miguu ambao wamekuja ofisini kwangu wakiongozwa  na Mwenyekiti wa BFA tuweze kujadili na kuweka misingi imara ambayo itawasaidia wachezaji wetu ambao wamepigana kufa na kupona katika kipindi chote na kufanikiwa kuwa mabingwa wa ligi daraja la tatu ngani ya Mkoa wa Pwani kwa hivyo tunapaswa kuwapa sapoti ya ina yake.

 

Katibu Tawala huyo amabye pia ni Mwenyekiti wa wa baraza la michezo Wilaya Bagamoyo alifafanua kuwa timu hiyo kwa sasa ipo katika maandalizi ya kujianda ana ligi ya mabingwa ngazi ya Taifa hivyo  serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa michezo inabidi tunaweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kwamba tunaweza kufika mbali zaidi na kupanda daraja la pili na hatimaye katika siku zijazo tuweze kushiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara.

“Hii timu imeweza kuutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani kwa hivyo kwa sasa inawakilisha Mkoa wa Pwani kwa ujumala japo inatokea Wilaya ya Bgamoja kitu kikubwa ninachowaomba wadau wote kwa pamoja tuungane na kutoa michango yetu ya fedha ambazo zitaweza kutumika katika mahitaji mbali mbali ya chakula kwa wachezaji pamoja na mambo mengine ya msingi kama mipira na jezi hivyo ninawaomba sana na nia yetu tushiriki ligi kuu ya Tanzania bara katika siku ya baadae,”alifafanua mgeni.  

  

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA) Olnjilie Maliwa  alisema kwamba lengo kubwa na kwenda kumtembelea katibu Tawala wa Wilaya hiyo juu ya timu yao ya soka y baga friends ambayo imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu katika ngazi ya Mkoa wa Pwani ili kuweza mikakati ambayo itasaidia kuweza kufika mbali zaidi katika hatua nyingine.

“Mimi kama Katibu wa BFA tumeweza kuongozana na uongozi wa kamati ya utendaji ya mabingwa wetu wa soka katika ligi daraja la tatu ambao ni timu ya Baga friends tukae kwa pamoja ili tuombe kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya michuano ya Taifa na lengo letu ni kuhakikishatimu hii inaweza kufanya vizuri na kufika hatua ya ligi daraja la pili katika msimu unaokuja”alisema Mwenyekiti  huyo.

Aidha Katika hatua nyingine alimponeza kwa dhati Katibu Tawala wa wilaya ya Bagmoyo kwa kuwa bega kwa bega katika kipindi chote cha michuano iliyopita hadi wameweza kufanikiwa kuibuka na ubingwa katika ligi hiyo daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani na kuwaomba wadau wengine wa soka katika maeneo mbali mbali kujitokeza kwa wingi ili kuipa sapoti ya kutosha timu yao ambayo ndio pekee inawakilisha Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Pages