NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
WATUMISHI
wa Umma wametakiwa kubadilika na kuacha kufanya kazi kimazoea na
badala yake wametakiwa kuzingatia Miiko na maadili ya uongozi.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Dkt Faustine Ndugulile alipokuwa akifungua mafunzo ya uongozi
kwa wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo jijini hapa na kusisitiza
maadili ya uongozi katika Utumishi wa umma.
Waziri
huyo amesema kuwa watumishi wa Umma wamejisahau katika utendaji kazi wa
majukumu yao ya kila siku mahala pakazi, badala ya kuhudumia Umma na
kujiona kama vile wanajihudumia wenyewe.
Amewataka
katika mafunzo hayo kufahamu dhana ya misingi ya uongozi kwa kuzingatia
Miiko na maadili ya uongozi, Sheria na taratibu za Utumishi wa
Umma,uongozi wenyetija na wakutatua changamoto ili kufikia Malengo na
kuwa na uwajibikaji wa pamoja.
"Mafunzo
Haya yamekuja katika muda sahihi kabisa na ukizingatia Wizara hii ni
mpya imeundwa Desemba, 5 2020, mtambuka ,ya kimkakati na inagusa nyanja
zote za kiuchumi na kijamii basi Hanna budi mpate mafunzo ya uongozi wa
kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania,"amesema Dkt Ndugulile.
Na
kuongeza kusema kuwa" Nimeelezwa kuwa mafunzo haya yanalenga kuwajenga
na kuwaimarisha ili muweze kuongeza buena kimkakati," Amesema.
Kwa
upande wake Mhandisi Kundi Mathew Naibu Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari amesema mafunzo hayo yanawapa muongozo namna ya
kwenda kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) .
Amesema
pia mafunzo hayo yanakwenda kuwakumbusha na kuwarudisha watumishi wa
Umma katika Wizara hiyo mpya na kuwarudisha katika misingi ya Utumishi
bora na wahaki.
Naye
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora Deogratius Ndejembi
amesema wamefungua jambo sahihi kuwaita wanachuo cha Utumishi Umma ili
kuwapiga msasa watumishi wa Wizara mpya ya Mawasiliano naTeknolojia ya
Habari.
Ndejembi amesema
chuo cha Utumishi wa Umma kipo kisheria na sio kama vyuo vingine kama
Chuo Kikuu cha UDOM, Mzumbe au Chuo cha Dar es Salamu UDSM.
"Chuo
hiki ni tofauti na vyuo vingine vya elimu ya juu mtu yoyote aliyemaliza
kusoma vyuo vya elimu ya juu na ni mtumishi wa Umma ni lazima apatiwe
mafunzo katika Chuo cha Utumishi wa Umma," amesema Ndejembi.
No comments:
Post a Comment