HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2021

NMB yazindua 'Bonge la Mpango' itakayomwaga zawadi za Mil. 550/-



Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi,  akiwa kwenye gari ya kifahari aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya Shilingi  milioni 169 itakayoshindaniwa  kwenye kampeni ya Weka Akiba na Ushinde  iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni maofisa wa benki hiyo. 


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde iitwayo Bonge la Mpango.



NA SALUM MKANDEMBA

BENKI ya NMB imezindua kampeni ya miezi mitatu iitwayo 'Bonge la Mpango,' itakayowawezesha wateja kushinda zawadi mbalimbali, zikiwamo pesa taslimu, pikipiki ya miguu mitatu, gari dogo la mizigo 'kirikuu' na gari ya kifahari aina ya Toyota Fortuner.

NMB Bonge la Mpango, kampeni itakayotoa zawadi zenye thamani ya Sh. Milioni 550, ni sehemu ya mkakati wa kuifanya benki hiyo kuendelea kuwa chaguo la kwanza la kwa wateja kwa usalama fedha zao pamoja na uhakika wa huduma za kibenki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi, aliitaja Bonge la Mpango, kuwa ni pampeni inayorejesha kwa wateja sehemu ya faida waliyopata katika mwaka wa 2020.

"Mwaka 2020 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa NMB, ambako licha ya kupata faida inayofikia Sh. Bilioni 205, pia tulitwaa Tuzo ya Benki Salama Zaidi Tanzania, tuliyopewa na Jarida la Global Financial.

"Bonge la Mpango, inakuwa kampeni ya kwanza kabisa kwa mwaka huu wa 2021, ambao tumepania kubaki juu kihuduma, na kuwazawadia wateja wetu wanaofikia zaidi ya milioni tatu kote nchini, pamoja na wateja wapya," alisema Mponzi.

Alibainisha kuwa, wateja watakaoweka pesa katika akaunti zitakazokuwa na akiba inayoanzia Sh. 100,000 na wateja watakafungua akaunti mpya na akiba na kianzio cha kiasi hicho, watajishindia zawadi za kila wiki na za kila mwezi.

Aliitaja zawadi ya kila wiki kuwa ni pesa taslimu Sh. 500,000 (wateja 10), na Pikipiki ya miguu mitatu aina ya Lifan Cargo, wakati zawadi za kila mwezi katika miezi mitatu ya kampeni hiyo itakuwa ni gari dogo la mizigo aina ya 'kirikuu.

"Zawadi kuu itakuwa ni gari la kifahari la Toyota Fortuner lenye thamani ya Sh. Milioni 169, ambayo itashindaniwa na wateja wenye akiba ya Sh. Milioni 10 kwenye akaunti zao iliyodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja (siku 30)

"Hiki ni kipindi cha mavuno kwa wateja wetu na kwa wale wasiokuwa nasi, watalazimika kufungua akaunti mpya na kuweka kianzio hicho ili kujiwekea nafasi ya kushinda," alisisitiza Mponzi.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema kanda yake imejipanga vya kutosha kuibeba kampeni hiyo ya NMB Bonge la Mpango na kuifikisha kwa jamii nayowahudumia kupitia matawi yaliyopo katika kanda hiyo.

"Waliokuwa wanajiuliza juu ya wapi mahala sahihi kuweka pesa zao, jibu lao ni NMB. Tunawakaribisha kuungana nasi ili kuwa sehemu ya familia pana inayojumuisha wateja wa NMB na pia kushiriki kampeni hii.

"Bonge la Mpango sio tu imebeba mrejesho wa faida yetu kwa wateja, bali pia ni uwezeshaji mkubwa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, ndio maana tuna zawadi za pesa taslimu, pikipiki ya miguu mitatu na gari dogo la mizigo," alisisitiza Richard.

Ukiondoa Bonge la Mpango, NMB kwa sasa iko katika siku za mwisho za kampeni ya NMB MastaBATA, inayohamasisha matumizi na manunuzi kwa Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, iliyozinduliwa Novemba 24 mwaka jana na kutarajia kufikia ukomo mwishoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

Pages