HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 10, 2021

OLE NASHA ASHIRIKI MKUTANO WA PILI KIKAO CHA NNE CHA BUNGE LA NNE LA AFRIKA MASHARIKI

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Ole Nasha akifuatilia Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kilichokuwa kikiendelea kwa njia ya video.

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Ole Nasha (Mb) ashiriki katika Mkutano wa Pili, Kikao cha Nne, Bunge la Nne la Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao. 

 

Kikao hicho kimefunguliwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga na baadaye kuendelea kuliongoza Bunge katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku. Shughuli ziliyofanywa na Bunge hilo na kufuatiliwa na Mhe. Ole Nasha ilikuwa ni kusomwa kwa mara ya kwanza Muswada wa Afrika Mashariki kuhusu Mifugo wa mwaka 2021, uwasilishwaji wa taarifa ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili ambayo inaangazia tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Kamisheni ya Bonde la Ziwa Viktoria na uwasilishwaji wa Hoja ya Azimio la Bunge la kulishawishi Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki kuhusu uharakishwaji wa kuanzisha mfuko wa dharura wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika Jumuiya. 

 

Bunge la Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake kwa njia ya mtandao ambavyo vitafanyika kwa kipindi cha wiki tatu kuanzia tarehe 28 Januari hadi 17 Februari 2021. 

No comments:

Post a Comment

Pages