HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2021

RAIS MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VITATU MKOANI MOROGORO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Ngozi cha Taifa-Morogoro Rostam Aziz wakati akifungua Kiwanda hicho cha Ngozi cha Taifa-Morogoro kilichopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kiwanda cha Ngozi cha Taifa kilichopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya hatua za uchakataji wa Ngozi katika Kiwanda cha Ngozi cha Taifa mara baada ya kukifungua.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ngozi ambayo imeshatengenezwa katika Kiwanda hicho cha Taifa kilichopo Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ngozi cha Taifa-Morogoro kilichopo Kihonda mkoani Morogoro.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao cha Mahashree Tanzania Limited kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kiwanda cha Kuchakata Mpunga cha MW Rice Millers limited kilichopo Kihonda mkoani Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya bidhaa za mchele wa aina mbalimbali katika Kiwanda cha MW Rice Millers limited mara baada ya kukifungua.

Sehemu ya Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kufungua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao cha Mahashree Tanzania Limited kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. PICHA NA IKULU.

 

No comments:

Post a Comment

Pages