Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt Leonard Akwilapo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Februari 5, 2021 kuhusu Wiki ya Maonesho ya Ubunifu wa Kisayansi na Teknolojia (MAKISATU) yanayotarajiwa kuanza Machi
20-26.
NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
SERIKALI
imesema inatambua na inaendeleza juhudi mbalimbali za wabunifu wote
waliokwisha tengeneza bunifu tofauti tofauti hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Leonard
Akwilapo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea
Wiki ya Maonyesho ya Ubunifu wa Kisayansi na Teknolojia (MAKISATU) Machi
20 mpaka 26 mwaka huu.
Dkt
Akwilapo amesema kuwa mwaka jana katika Maonesho hayo ya MAKISATU Jumla
ya Wabunifu 1066 walijitokeza ambapo wabunifu 130 wote wanaendelezwa na
Serikali.
"Huu ni mwaka
wa Tatu kufanya Maonesho haya na lengo kubwa la Maonesho haya ya Sayansi
na Teknolojia MAKISATU ni kuwatambua wabunifu wote waliopo hapa
Tanzania na kuendeleza juhudi mbalimbali za wabunifu hao bila kusahau
kuwa ni moja ya ajira," amesema Dkt Akwilapo.
Amesema
usajili kwa wabunifu umeanza toka November 18 ,2020 na kumalizika
February 2021 ambapo wizara inayoratibu na kushirikiana.
Aidha
ametoa wito kwa watu mbalimbali na wabunifu wenyewe kuchangamkia fursa
katika Maonesho hayo ya MAKISATU March 2021 na ambapo kutakua na
Maonesho mbalimbali ya Teknolojia na Ubunifu.
MIKAKATI.
Amesema
mikakati ya mwaka huu ni pamoja na wadau wa Ubunifu Katika masuala ya
Sayansi na Teknolojia kuanzisha vikundi vitakavyowatambua wabunifu
kuanzisha utaratibu kuanzia Serikali za Mitaa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Tume ya sayansi na Teknolojia Dkt Amos Nungu
Amesema huu ni mwaka wa tatu wa mashindano hayo ambapo wamefanikiwa
kuwaongezea uelewa wabunifu wote waliochukulia na Serikali.
Aidha amesema wabunifu hao wote wamepewa mafunzo na kuendelezwa kulingana na bunifu zao.
Hata
hivyo maadhimisho hayo yatawachukua wanafunzi kuanzia shule ya msingi,
sekondari vyuo vya ufundi stad vyuo vikuu na Taasisi kutoka mfumo usio
rasmi na maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo sayansi
Teknolojia kwa uchumi endelevu.
No comments:
Post a Comment