Timu ya Masoko na Uhusiano iliongozwa na Mkurugenzi wa Masoko wa UTT AMIS, Daud Mbaga (kulia), ilipomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai (wa pili kushoto) na kujadiliana kuhusu shuguli za Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS. Kushoto ni Afisa wa UTT AMIS kutoka Dodoma, Ahmed Salim na Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Martha Mashiku.
Timu ya wataalamu watakaotoa elimu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wabunge na watumishi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akiwa katika banda la Kampuni ya UTT AMIS iliyopiga kambi katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment