Katibu Mkuu wa Taasisi ya Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), Hassan Mohammed (EBS).
NA SULEIMAN MSUYA
KAMATI
ya Utendaji ya Taasisi ya Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE),
imeunda kamati ndogo nne ambazo zitashirikiana na kamati kuu kufanikisha
mipango ya taasisi hiyo kufikiwa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa SJTE, Hassan Mohammed
(EBS), amesema kamati hizo ndogo zimeundwa baada ya wajumbe wa kamati
hiyo kukutana kwa mara ya kwanza siku chache baada ya kuchaguliwa.
"Kamati
Tendaji ya SJTE ilifanya kikao cha kwanza chini ya Mwenyekiti Patrick
Mwanakatwe na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuunda kamati, kuteua
mweka hazina na uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya utendaji," amesema.
Katibu
mkuu huyo amesema pamoja na Mwenyekiti pia kikao hicho alikuwepo Makamu
Mwenyekiti James Tindi, Naibu Katibu Asha Kigundula, Mweka Hazina
Zaitun Dagila, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Nunu Rashid, Mussa Mongi na
Laurencia Sahani.
Katibu
mkuu amezitaja kamati zilizoundwa na Kamati ya Utendaji ni Kamati ya
Nidhamu na Maadili itakayoongozwa na Mwenyekiti Hassan Mbilili, wajumbe
Mhandisi Said Khalfan,
Jasmin Badar na Faraj Kimonge.
"Kamati ya Habari, Matukio na Safari ikuwa chini ya Mwenyekiti Seperatus Kisimba, Katibu Seleman Msuya, wajumbe Asha Kigindula Laurencia Sahani, Cecy Mushi, Adrian Galid, Jacob Mandeje, Leonard Ngomai, Mussa Mongi Chacha Sadalla na Alice Mgaya," amesema.
Aidha
Katibu Mkuu ametaja kamati nyingine ni ya Fedha, Uchumi na Mipango
chini ya Mwenyekiti Mashaka Kirazi, Katibu Zaituni Dagilla, wajumbe Nunu
Rashid, Masoud Ameir, Danny Poul, Dullah Dumea na Dk. Fanuel.
Amesema pia wameunda Baraza la Wadhamini ambalo litaongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Said Khalfan, Katibu
Rahim Varisanga, wajumbe Faraj Kimonge Hassan Mbilili na Nassor Ossama.
Amesema matarajio yao ni kuona kamati hizo ndogo zitashirikiana na Kamati ya Utendaji kusukuma gurudumu la maendeleo.
Mohammed
amesema kikao kilitoa maazimio kuwa nafasi mbili za wajumbe wa kamati
ya utendaji zijazwe kwenye mkutano unaotarajiwa kufanyika hivi
karibuni.
"Wajumbe
walikubaliana nafasi hizo ziachwe wazi mpaka utakapofanyika mkutano mkuu
ujao ili zijazwe kwa wagombea kupigiwa kura na wanachama wenyewe.
Hivyo nafasi hizo ziko wazi na zitatangaziwa utaratibu wa kuzijaza wakati wa mkutano ujao," amesisitiza.
Amesema
kuhusu nafasi ya mweka hazina wajumbe wa kamato tendaji kwa kauli moja
walikubaliana kuwa Zaituni Dagilla aendelee kuwa Mweka Hazina wa Simba
Jamii mpaka utakapofanyika mkutano ujao na kusomwa mapato na matumizi
ndio nafasi hiyo inaweza kufanyiwa mabadiliko ama la.
No comments:
Post a Comment