HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 02, 2021

BITEKO AZINDUA MAGARI SITA KWA AJILI YA TAFITI ZA MADINI

HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amezindua Magari sita kwa ajili ya kufanikiwa Tafiti za Madini nchini, Magari yenye thamani ya Sh. Milioni 950.

Amesema Sehemu kubwa ya uchimbaji wa madini inategemea utafiti wa Giololojia katika kuhakikisha mambo yote yaende kama ilivyopangwa na ili Watu wafike eneo husika (Site) Lazima kuwepo magari.

Akizungumza kabala ya kukabidhi magari hayo leo Februari 2, 2021 jijini Dodoma Waziri Biteko amesema uwepo wa maabara pia unaitajika ingawa tunayo maabara ya kisasa inayotambulika na kukabidhiwa cheti cha kutambuliwa kama maabara inauwezo . 

Amewataka kutambua Magari hayo hayatakuwa nafaida kama sekta ya madini haitaongeza mchango wake kutoka tuliko asilimia 5.2 mpaka kufika asilimia 10.

"Hesabu tunayotakiwa kumpeleka aliyetuteua ambaye ni Rais John Magufuli ni kumuonyesha kwamba tulikuwa sehemu fulani na tumesonga mbele sehemu kadhaa,"

Na kuongeza kuwa "Malengo yenu tuliyoyaweka katika Mapato ni kwamba  Mapato yenu kwa mwaka ni Milioni 500 Kwa mwaka hivyo ninatamani Sana kuona mnavuka hilo lengo," amesema Waziri Biteko.

Amesema kama tumeshapata  magari na tumeshategeneza maabara nzuri tena za kisasa tusije shuka kinapata Mapato yakishuka wote hapa tutaonekana hatuna maana. 

Aidha amewataka watumishi hao kuelewa kwamba hawapimwi kwa uwepo wa vifaa bali tunapimwa kwa uwepo wa matokeo na matokeo ni pamoja na wachimbaji wa madini wapate huduma za ugani.

" Na hiyo huduma ya Ugani kwa wachimbaji tuwafuate huko huko na kuanzia sasa tuachane na habari za kukaa maofisini kama changamoto ilikuwa ni magari basi magari ndio hayo hapo tumesha yapata hatuna visingizio tena," Amesema  Waziri Biteko

Hata hivyo amewataka Madereva watakaopewa kazi ya kuendesha magari hayo kuyatunza magari hayo na maafisa watakaokuwa wanakwenda Site wawe na wajibu wajibu wa kuyatunza magari .

"Nitasikitika mno nikiona baada ya muda magari haya yako juu mawe eti yameharibika magari hayo yanakila Aina ya nyenzo hata mkikwama mahali zipo nyenzo za kujinasua.", amesema Biteko.

Kwa upande wake mtendaji Mkuu  Taasisi ya Giololojia na Utafiti Tanzania  (GST) Dkt Mussa Budeba amesema
Kupatikana kwa magari hayo itakuwa rahisi kwao kwani kwani kazi kubwa ni kuchunguza.

Amesema kama inavyofahamika Madini yanapatikana Sehemu zenye mapori hivyo kuletwa kwa magari hayo itarahisisha kazi kwani hapo awali ilikuwa ngumu katika suala zima la usafiri.

No comments:

Post a Comment

Pages