HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 18, 2021

Mshindi droo ya pili NMB Bonge la Mpango akabidhiwa zawadi


Mshindi wa droo ya pili ya Kampeni ya NMB Bonge la Mpango - Yusuf Kyando akipokea funguo za Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan Cargo kutoka kwa  Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro  wakati wa hafla iliyofanyika katika Tawi la NMB mjini Tanga. Akishuhudia ni  Meneja wa Tawi la NMB Tanga - Elizabeth Chawinga.

 
Mshindi wa droo ya pili ya Kampeni ya NMB Bonge la Mpango - Yusuf Kyando akiwasha Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan Cargo baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro  wakati wa hafla iliyofanyika katika Tawi la NMB mjini Tanga. Akishuhudia ni  Meneja wa Tawi la NMB Tanga - Elizabeth Chawinga.
 
 
Na Mwandishi Wetu
 
 

Benki ya NMB kupitia kampeni yake ya Bonge la Mpango imekabidhi zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu aina ya Lifan Cargo kwa mshindi wa droo ya pili ya kampeni hiyo Yusuph Kyando mkazi wa Mombo wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

 

 Pikipiki hiyo inagharimu sh. milioni 4.4 ambapo tangu kuanza kwa kampeni hiyo mwezi Februari mwaka huu zawadi zinazogharimu zaidi ya shilingi milioni 35.2 zimetolewa ikiwemo fedha taslimu na pikipiki sita za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Aikansia Muro alisema, zaidi ya shilingi milioni 550 zimetengwa kwa ajili ya kampeni hiyo na kampeni hiyo ni maalum kwa ajili ya kurejesha faida kwa wateja wa benki hiyo pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa watanzania.

 

Kwa upande wake mshindi wa Bonge la Mpango Yusuf Kyando alisema amefurahi kupata zawadi hiyo gari mpya aina ya Toyota Fortuner fedha kwenye akaunti zao ili kujiongezea nafasi ya kuweza kushinda zawadi za Bonge la Mpango kama yeye alivyobahatika, kwani kuna fedha taslimu kuanzia sh.100,000 mpaka 500,000, pikipiki aina ya miguu mitatu aina ya Lifan Cargo, gari ya mizigo maarufu kama Kirikuu na gari mpya aina ya Toyota Fortuner zote zinashindaniwa.

 

Baada ya hafla hiyo ya makabidhiano, droo ya tatu ya kampeni hiyo iliyofanyika katika Tawi la NMB Tanga na washindi wengine 11 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejipatia fedha taslimu pamoja na washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo.


No comments:

Post a Comment

Pages