NA ASHA MWAKYONDE
DIWANI wa Kata ya Tandale iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Chifu Abdallah Saidi amesema hivi karibuni wanatarajiwa kuandaa mashindano yenye lengo la kukuza vipaji vya vijana katika kata hiyo.
Akizungumza jijini Dar Dar es Salaam amesema kuwa mashindano hayo yatahusisha mpira wa miguu, Pete, rede na michezo mingine mingi ikiwa ni pamoja na mchWEezo wa ngumi.
Ameongeza kuwa kupitia mashindano hayo wanatarajia kupata kupata vijana wenye vipaji wa michezo hiyo ambayo wataviendeleza ili viwasaidie katika maisha yao.
" Niliahidi kutengeneza nyumba ya kukuza vipaji vya vijana wa Tandale ( House of Talent), na baadae waweze kujiajiri wenyewe kupitia vipaji vyao, " amesema.
Chifu Saidi amesema kuna baadhi ya vijana hapa hapa nchini maisha yao yanategemea vipaji vyao ambapo aliwatolea mfano Hashim Thabiti na Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment